Nenda kwa yaliyomo

Nyoka-kijiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Thelotornis)
Nyoka-kijiti
Nyoka-kijiti kusi (Thelotornis capensis)
Nyoka-kijiti kusi (Thelotornis capensis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Colubridae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Oppel, 1811
Nusufamilia: Colubrinae
Jenasi: Thelotornis
A. Smith, 1849
Ngazi za chini

Spishi 4:

Nyoka-kijiti ni spishi za nyoka wa jenasi Thelotornis katika familia Colubridae. Wakikaa tuli mtini wanafanana na kijiti au kitawi kilichokauka.

Nyoka hawa ni wembamba sana na warefu kiasi: kwa wastani sm 90-130 na kipeo cha m 1.4-1.6 kulingana na spishi. Kichwa kina umbo wa mshale na mboni zina umbo wa tundu la ufunguo. Rangi yao ni kijivu au kahawia lakini kichwa ni kijani kabisa au juu yake tu.

Nyoka-kijiti huishi mitini ambapo huwinda mijusi, vyura na ndege wadogo. Mara nyingi hukaa chini kiasi ili waweze kushambulia mawindo yaliyo ardhini.

Chonge zao ni meno ya nyuma kabisa lakini wanaweza kuingiza sumu waking'ata mtu. Kwa bahati nzuri nyoka hawa ni waraufu na hawang'ati kwa kawaidi. Hata hivyo sumu hii ni toksinidamu kali na hakuna makata na mara nyingine watu hufa baada ya kuumwa. Nyoka hawa wakitishwa shingo yao inafura na kuonyesha mabaka meusi au kahawia.

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-kijiti kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.