Tasbihi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tasbihi ya Fatura ya Waosmani.

Tasbihi (kutoka neno la Kiarabu تَسْبِيح, Tasbīḥ, ambalo linategemea kauli "Subhan'allah") katika Uislamu ni aina ya sala (dhikr) inayofanyika kwa kukariri maneno machache kwa sifa na utukufu wa Allah.

Ili kutunza hesabu ya kauli hizo, vinatumika ama mifupa ya mkono wa kulia ama punje zilizounganishwa katika kamba au uzi (misbaha) inayofanana na ile ya dini nyingine, k.mf. ya Wakristo Waorthodoksi (kamba ya sala) na Wakatoliki (rozari).

Shanga zilitumika kama pambo tangu kale: barani Afrika zimepatikana za miaka 10,000 KK.

Lini na wapi zilianza kutumika kwa ajili ya sala haijulikani, lakini kuna sanamu ya karne ya 3 KK inayomuonyesha Mhindu akiwa na ushanga wa sala.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Dubin, L. S. (2009). Prayer Beads. In C. Kenney (Ed.), The History of Beads: From 100,000 B.C. to the Present (Revised and Expanded Edition) (pp. 79–92). New York: Abrams Publishing.
  • Henry, G., & Marriott, S. (2008). Beads of Faith: Pathways to Meditation and Spirituality Using Rosaries, Prayer Beads and Sacred Words. Fons Vitae Publishing.
  • Untracht, O. (2008). Rosaries of India. In H. Whelchel (Ed.), Traditional Jewelry of India (pp. 69–73). New York: Thames & Hudson, Inc.
  • Wiley, E., & Shannon, M. O. (2002). A String and a Prayer: How to Make and Use Prayer Beads. Red Wheel/Weiser, LLC.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.