Nenda kwa yaliyomo

Suraiya Khanum

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Suraiya Khanum (ikitamkwa pia Surraiya Khanum) ni mwimbaji mkongwe toka Punjab. Pia anajulikana kwa maonyesho yake yenye kusuza roho na akiimba muziki wa Sufi kwenye Televisheni ya Pakistan na vituo vingine.[1][2]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Suraiya Khanum alianza kazi yake ya uimbaji kwenye redio ya Pakistan Radio Multan iliyoko Multan, Pakistan mwaka 1977. Kimuziki alishawishiwa na Ustadhi Muhammad Juman. Ustadhi Nusrat Fateh Ali Khan alimpatia mafunzo kwa miaka 8 na pia alipatiwa mafunzo rasmi na Ustadhi Faiz Ahmed kwa miaka 21. Kimuziki ameshawishiwa na mwanamuziki mkongwe Tufail Niazi pia Reshma na Iqbal Bano.[3] Alionekana kwenye awanu ya nane ya mfululizo wa kipindi halisia cha muziki cha televisheni Coke Studio Pakistan kama msanii mshirikishwaji . Aliimba [4][5] wimbo maarufu wa harusi na ambao uliimbwa na msanii mkongwe Tufail Niazi "Chirya Da Chamba" akiwa pamoja na Anwar Maqsood uliopongezwa kwa utungwaji na usimulizi mzuri wa barua uliyofanywa na Anwar Maqsood. Ilisemwa kuwa wimbo "uliweka kumbukumbu isiyofutika kwa mashabiki".[1]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Nyimbo[hariri | hariri chanzo]

 • MenDa Ishq Vi Toon (wimbo wa Kikafi umeandikwa karne ya 19 na mshairi wa Kisufi, Khawaja Ghulam Farid). Huu wimbo una historia ndefu na uliimbwa hapo awali na Inayat Hussain Bhatti na Pathanay Khan
 • Toonba – Turr Multanon Toonba Aaya
 • Raataan Jaagni Aan
 • Yaar Toon Kithay Vain
 • Way Main Chori Chori Tere Naal La Layyan Akhhaan Wey (wimbo wa Kipunjabi umeandikwa na mshairi Manzoor Hussain Jhalla)
 • Ramzaan KehRay Velay Laaiyan
 • Mera Chann Masta
 • Bhul Jaania Kisay De Naal Pyaar Na
 • Saaiyaan
 • Bol Mitti Daya Baawia (uliimbwa kwa mara ya kwanza na Alam Lohar)

Coke Studio (Pakistan)[hariri | hariri chanzo]

 • Chiryan Da Chamba (2015) (onyesho la wimbo pia akimshirikisha msomaji Anwar Maqsood)[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. 1.0 1.1 "Pakistani singing talent at its best". The Daily Times. 26 Agosti 2015. Iliwekwa mnamo 20 Januari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 2. Surriya Khanum performing on Coke Studio, Pakistan, videoclip on YouTube Published 22 August 2015. Retrieved 20 January 2019
 3. Suraiya Khanum profile on Coke Studio (Pakistan) Retrieved 20 January 2019
 4. 4.0 4.1 "Coke Studio: Will songs from Episode 2 make it to your wedding soundtrack?". Pakistan: Dawn. 21 Agosti 2015. Iliwekwa mnamo 20 Januari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 5. Ali Raj (24 Agosti 2015). "Coke Studio Season 8-Episode 2: Sugar, spice and some things nice". The Express Tribune (newspaper). Iliwekwa mnamo 20 Januari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Suraiya Khanum kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.