Nenda kwa yaliyomo

Subway Surfers

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Subway Surfers ni mchezo wa video wa kukimbia usio na mwisho. Mchezo huu uliundwa na Kiloo na SYBO, kampuni za binafsi zinazopatikana nchini Denmark. Unapatikana kwenye simu za Android, iOS, Kindle, na Windows.

Katika mchezo huo, mchezaji huchukua jukumu la wahuni wa graffiti ambao, wanapokutwa na polisi kwenye kitendo cha kutumia graffiti kwa kuchora alama na kuchafua reli ya metro, wanakimbizwa kwenye njia za reli ili kumtoroka polisi na mbwa wake. Wanapokuwa wanakimbia, wanakusanya sarafu za dhahabu, nguvu za kuruka na vitu vingine. Mchezaji huendelea kikimbia mpaka atakapokutana na kizuizi kisichokwepeka.

Subway Surfers ilitolewa mnamo 24 Mei 2012 na visasisho (updates) kulingana na likizo za msimu. Tangu Januari 2013, visasisho vinatokana na mandhari ya Dunia, ambayo husasisha mpangilio wa mchezo kila baada ya wiki tatu au nne, kawaida katika siku za wikendi.

Mnamo mwaka 2017, Subway Surfers ilikuwa mchezo uliopakuliwa zaidi kuliko yote ulimwenguni. Mnamo Machi 2018, Subway Surfers ikawa mchezo wa kwanza kwenye Duka la Google Play kuvuka kizingiti cha kupakuliwa yaani bilioni moja. Mnamo Mei 2018, Subway Surfers walivuka alama ya kupakuliwa ya bilioni mbili.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Subway Surfers kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.