Nenda kwa yaliyomo

Kwenzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sturnus)
Kwenzi
Kwenzi maridadi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Muscicapoidea (Ndege kama shore)
Familia: Sturnidae (Ndege walio na mnasaba na kwenzi)
Rafinesque, 1815
Spishi: Angalia katiba
Ngazi za chini

Jenasi 33:

Kwenzi au kuzi ni ndege wadogo kiasi wa familia Sturnidae. Spishi nyingine zinaitwa kizole au nyangala. Wanatokea Ulaya, Afrika, Asia na Australia. Baadhi ya spishi zimewasilishwa katika Amerika ya Kaskazini, Nyuzilandi na Afrika. Wanapenda kuwa kwa makundi. Spishi nyingi zina rangi ya buluu, pengine pamoja na rangi kali kama nyekundu, machungwa na njano; spishi nyingine ni nyeusi, kijivu au kahawia, pengine pamoja na nyeupe, njano, nyekundu au pinki. Sauti yao ina utata na huiga sauti za mazingira, kama ndege wengine, kamsa za magari na hata msemo wa binadamu. Ndege hawa hula wadudu na matunda hasa, lakini hula nusra kila kitu. Takriban spishi zote hulijenga tago lao katika tundu. Jike huyataga mayai 2-6 meupe au buluu.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za kabla ya historia

[hariri | hariri chanzo]
  • Aplonis diluvialis (Huahine Starling) (Mwisho wa Quaternary)
  • Aplonis sp. undescr. (Erromango Starling) (Mwisho wa Quaternary)