Spidometa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Spidometa
Spidometa.

Spidometa (kutoka Kiingereza "speedometer") ni aina ya kipimio kinachoonesha kiasi cha kasi ya gari linavyosonga.

Kwa kawaida inaonyesha kasi ya maili kwa saa (mph) kwa nchi ambazo hutumia umbali wa maili au Kilomita kwa saa (kph) kwa nchi zinazotumia mfumo wa meta kwa umbali.

Mwanzoni, spidometa ilikuwa chaguo ambalo wamiliki wa gari waliweza kuchagua kununua na kupachika kwenye magari yao. Kuanzia mwaka wa 1910 ilijengwa katika magari yote.