Nenda kwa yaliyomo

Caesi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sizi)


Caesi (Caesium)
Caesi tupu ina rangi kifedha-nyeupe inayobadilika kuwa kidhahabu ikiguswa na kiasi kidogo sana cha oksijeni kama inavyopatikana katika kioo cha testitubu; hutunzwa katika gesi adimu
Caesi tupu ina rangi kifedha-nyeupe inayobadilika kuwa kidhahabu ikiguswa na kiasi kidogo sana cha oksijeni kama inavyopatikana katika kioo cha testitubu; hutunzwa katika gesi adimu
Jina la Elementi Caesi (Caesium)
Alama Cs
Namba atomia 55
Mfululizo safu Metali alikali
Uzani atomia 132.9054519
Densiti 0.89
Ugumu (Mohs) 0.2
Kiwango cha kuyeyuka 301.59 K (28.44  °C)
Kiwango cha kuchemka 944 K (671 °C)
Asilimia za ganda la dunia 6 · 10-4 %
Hali maada mango

Caesi ni elementi na metali alikali yenye namba atomia 55 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 132.9054519. Alama yake ni Cs. Jina linatokana na Kilatini "caesius" linalomaanisha buluu kwa sababu ya mistari taswirangi yake iliyo upande wa buluu ya taswirangi.

Caesi ni metali yenye kiwango cha kuyeyuka duni sana ya 28 °C, hivyo hutokea kama kiowevu kwa halijoto ya chumbani tayari. Ni dutu inayomenyuka sana kwa hiyo haitokei kwa umbo safi kiasili bali kwa kampaundi mbalimbali. Kati ya elementi zote mmenyuko wake ni mkali baada ya Florini. Kwa sabu hiyo Caesi hupaswa kutolewa katika maabara na hutunzwa ndani ya gesi adimu kama arigoni.

Matumizi yake ni katika saa atomia, vyoo kwa teknolojia ya inforedi na kwa injini ya ioni kwa anga-nje.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Caesi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.