Nenda kwa yaliyomo

Siyaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Siyaya wakiwa stejini.

Siyaya kwa jina maarufu Siyaya Arts ni kikundi cha muziki, kucheza na kuigiza kutoka Makokoba, Bulawayo, Zimbabwe.

Siyaya ilianzishwa mwaka wa 1989 na awali ilijulikana kama Nostalgic Actors and Singers Alliance (NASA).[1][2] Ilianzishwa na wanachama 5 wakiongozwa na Mike Sobiko. Kuanzishwa kwake kulichangiwa na hadithi za kitamaduni, muziki na densi zinahusiana na jiji la Bulawayo.[3]

Wanachama wamekuwa wakibadilika mara kwa mara huku wanachama wengi wa zamani wakiendelea na miradi mingine kama hiyo. Safu hiyo sasa ina wanachama 13 chini ya uongozi wa Saimon Mambazo Phiri. Katika maadhimisho ya miaka 10 walibadilisha jina lao kuwa Siyaya (jina la Kindebele lenye maana ya "on the move" kwa kiingereza).[4]

Kundi hili limefanya ziara nyingi barani Ulaya na Afrika na kujipatia sifa nzuri hasa kwa kugusa masuala ya kijamii katika muziki wake.

Matamasha

[hariri | hariri chanzo]

Siyaya wametumbuiza kote barani Afrika na Ulaya.[5] Baadhi ya matamasha waliyohudhulia tangu 1993 ni pamoja na Aberdeen International Youth Festival (Uskoti), Towersey Festival (Uingereza), Glastonbury Festival (Uingereza), Pontardawe Festival (Welisi), Waterford Spraoi (Eire), WOMAD Reading Festival (Uingereza), Malopo Tamasha (Pretoria, Afrika Kusini), Edinburgh International Fringe Festival (Uskoti), Market Theatre Community Theatre Festival (Afrika Kusini), Ross On Wye International Festival (Welisi), Scena Church & Theater Festival (Hanover Ujerumani), Panafest Historic Theatre Festival (Cape Coast, Ghana), Streets Ahead Festival Manchester (Uingereza), Sidmouth International Folk Festival (Uingereza), Earagail Arts Festival (Eire) na mengine mengi.[6]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
  • Yebo! Yes! (2000)
  • Kokoba Town (2002)
  • Futhi Njalo (2009)
  • Zambezi Express (2012)[7]
  1. The Chronicle. "Siyaya 25 years in arts". The Chronicle (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2022-07-29.
  2. The Sunday News. "Siyaya Arts collabos with Hawaiian trio". The Sunday News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2022-07-29.
  3. "Siyaya Arts". Music In Africa (kwa Kiingereza). 2015-07-06. Iliwekwa mnamo 2022-07-29.
  4. "Artist Profiles: Siyaya | World Music Central" (kwa American English). 2016-12-19. Iliwekwa mnamo 2022-07-29.
  5. "Siyaya's Zimbabwean rhythms get the masses moving at Womad UK". The South African (kwa Kiingereza). 2014-07-29. Iliwekwa mnamo 2022-07-29.
  6. "Siyaya Arts". Pindula (kwa Kiingereza). 2020-06-25. Iliwekwa mnamo 2022-07-29.
  7. About the Author Editor Twitter Facebook Email. "Siyaya Arts releases fourth album" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-14. Iliwekwa mnamo 2022-07-29. {{cite web}}: |author= has generic name (help)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: