Sista Blandina
Mandhari
Sista Blandina (jina la kuzaliwa: Rosa Maria Segale; Cicagna, Genova, Italia, 23 Januari 1850 – Cincinnati, Marekani, 23 Februari 1941),[1] alikuwa mtawa wa Shirika la Masista wa Upendo la Cincinnati na mmisionari, ambaye alipata umaarufu kutokana na utumishi wake kwenye mipaka mipya ya Marekani mwishoni mwa karne ya 19.[2]
Wakati wa kazi yake ya kimisionari, alikutana na watu maarufu kama Billy the Kid na viongozi wa makabila ya asili ya Marekani, ikiwa ni pamoja na Waapache na Wakomanche. Alifanya kazi kama mwalimu na mfanyakazi wa kijamii katika maeneo ya Ohio, Colorado, na New Mexico, akiwasaidia Waindio, walowezi wa Kihispania, na wahamiaji kutoka Ulaya.[3]
Imeanzishwa kesi ya kumtangaza mtakatifu[4].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Servant of God Blandina Segale, SC - Sisters of Charity of Cincinnati". Iliwekwa mnamo 5 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Sister Irene Hartman, O.P. "Sister Blandina Sagale SC; 1850-1941". dcdiocese.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 8, 2008. Iliwekwa mnamo 31 Oktoba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ The Nun Who Took on Billy the Kid - Katie O'Brien Catholic Heritage
- ↑ "'Fastest nun in the west' Blandina Segale on path to sainthood", The Australian, June 26, 2014. Retrieved on 31 October 2014.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |