Severi wa Trier
Mandhari
Severi wa Trier (alifariki Trier, leo nchini Ujerumani, karne ya 5) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 445/446[1][2][3][4][5][6] hadi kifo chake, labda mwaka 451, Wahunni walipoangamiza Trier[7].
Mwanafunzi wa Lupo wa Troyes katika monasteri ya Lerins, Ufaransa, baada ya kupewa uaskofu aliongozana na Jermano wa Auxerre hadi Britania kupinga uzushi wa Upelaji, halafu aliinjilisha makabila ya Wagermanik[8].
Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 15 Oktoba[9].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hans Hubert Anton: studies on the social and ecclesial leadership Gaul: Germanus of Auxerre, Lupus of Troyes and the Trier bishops of the 5th century (Yearbook for West German national history 19 Jg 1993) p.17-40.
- ↑ Hans Hubert Anton: Trier in the Middle Ages Paderborn, Munich, and others, 1987 82f.
- ↑ Friedrich Prinz: European Basics of German history (4th-8th century.) (Handbook of German History, 10th edition, Stuttgart 2004), p 399.
- ↑ Full Holy lexicon, Volume 5. (Augsburg 1882), p279.
- ↑ Trier at New Advent.org.
- ↑ Diocese of Trier at GCatholic.org.
- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/91894
- ↑ Severus is written about in the late antiquity Vita of Germanus of Auxerre, and mentioned around 480 by Constantine of Lyon. Furthermore, he also appears in the Life of Lupus of Troyes and the Ecclesiastical History of the Venerable Bede. These combined works brought together the previously separate reports on the journey to Britain and the German Mission. In his research, Wilhelm Levison has been skeptical about the identification of the Severus with these missions. However other researchers, such as Eugen Ewig, disagree. Here they found value in the Vita of Lupus. But the question remains whether the vita is contemporary. For many writers, the doubts have now been dispelled. Hans Hubert Anton has examined the sources again critically and concludes that the Vita of Lupus must be nearly contemporary. The travel to Britain he considers plausible.
- ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |