Nenda kwa yaliyomo

Senzo Mazingiza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Senzo Mazingiza
[[File:
Senzo Mazingiza
|frameless|alt=]]
Jina la asiliSenzo Mbatha
AmezaliwaSenzo Hamillton Mazingiza
11 May, 1979, Afrika ya kusini
UtaifaAfrika ya Kusini
Kazi yakeMpira wa Miguu
AsasiYanga Sc
Anajulikana kwa ajili yakombe la Dunia La FIFA 2010

Senzo Hammilton Mazingiza (jina halisi: Senzo Mbatha; amezaliwa nchini Afrika ya Kusini, 11 Mei 1979) ni kiongozi na mtaalamu wa masuala ya michezo kutoka Afrika ya Kusini. Mazingiza alijitwalia umaaarufu mkubwa wakati wa michuano ya "Kombe la Dunia La FIFA 2010" iliyokuwa ikifanyika nchini mwake[1].

Mazingiza aliwahi kuwa mkurugenzi mkuu wa timu ya mpira wa miguu Simba S.C. nchini Tanzania, na kwa sasa ni mshauri mkuu wa timu ya mpira kutoka Tanzania Yanga S.C..

Kazi

Mazingiza alifanya kazi kama mkurugenzi mkuu wa timu ya mpira ya Chuo kikuu cha Pretoria nchini Afrika ya Kusini kati ya mwaka 2000 mpaka 2004.

Baada ya kufanya kazi na timu ya chuo kikuu hicho kwa muda mrefu, Mazingiza alijiunga na timu ya mpira ya Bay United F.C hukohuko Afrika ya Kusini.

Mazingiza ni mmoja ya watu waliochaguliwa kwenye kamati ya uongozi wa kombe la Dunia La FIFA 2010 huko Afrika ya Kusini[2].

Mazingiza amewahi kuwa mkurugenzi mkuu katika timu ya Simba ambapo amefanya kwa muda wa mwaka mmoja.

Mazingiza kwa sasa ni mshauri mkuu, katika timu ya Yanga.[3]

Marejeo

  1. World Football Summit (2020-03-02). "Senzo Mbatha: "WFS is an opportunity to learn new ideas and meeting new partners"". World Football Summit (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2020-10-01.
  2. Daniel Mothowagae. "Flying the flag beyond our borders". Citypress (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-10-01.
  3. Majuto Omary (2020-08-10). "Tanzania: Senzo Joins Yanga After Shock Exit From Simba". allAfrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-10-01.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Senzo Mazingiza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.