Sengi
Sengi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Isanje (Petrodromus tetradactylus)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 4:
|
Sengi, njule au isanje ni wanyama wadogo wa familia Macroscelididae. Jina la njule litumika kwa jenasi Rhynchocyon na isanje litumika kwa Petrodromus tetradactylus. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara katika maeneo mbalimbali. Sifa bainifu mno ya sengi ni pua yao refu sana ambayo wanaweza kuipota ili kutafuta chakula. Hii inafanana kidogo na mwiro wa tembo na ni chimbuko cha jina lao la Kiingereza "elephant shrew". Miguu yao ni mirefu kwa kulinganisha na huenda wakirukaruka kama sungura. Rangi yao ni kahawia au kijivu kwa kawaida lakini spishi nyingine zina rangi kali pia kama nyekundu au njano. Hula invertebrata kama wadudu, buibui, majongoo, tandu na nyunguyungu.
Spishi[hariri | hariri chanzo]
- Elephantulus brachyrhynchus, Sengi Pua-fupi (Short-snouted Elephant Shrew au Sengi)
- Elephantulus edwardii, Sengi-rasi (Cape Elephant Shrew au Sengi)
- Elephantulus fuscipes, Sengi Miguu-myeusi (Dusky-footed Elephant Shrew au Sengi)
- Elephantulus fuscus, Sengi Mweusi (Dusky Elephant Shrew au Sengi)
- Elephantulus intufi, Sengi-nyika (Bushveld Elephant Shrew au Sengi)
- Elephantulus myurus, Sengi-mawe Mashariki (Eastern Rock Elephant Shrew au Sengi)
- Elephantulus pilicaudus, Sengi-mawe wa Karuu (Karoo Rock Elephant Shrew au Sengi)
- Elephantulus revoili, Sengi Somali (Somali Elephant Shrew au Sengi)
- Elephantulus rozeti, Sengi Kaskazi (North African Elephant Shrew au Sengi)
- Elephantulus rufescens, Sengi Kahawiachekundu (Rufous Elephant Shrew au Sengi)
- Elephantulus rupestris, Sengi-mawe Magharibi (Western Rock Elephant Shrew au Sengi)
- Macroscelides flavicaudatus, Sengi Masikio-mafupi wa Namibia (Namib Short-eared Elephant Shrew au Sengi)
- Macroscelides micus, Sengi Masikio-mafupi wa Etendeka (Etendeka Short-eared Elephant Shrew au Sengi)
- Macroscelides proboscideus, Sengi Masikio-mafupi wa Karuu (Karoo Short-eared Elephant Shrew au Sengi)
- Petrodromus tetradactylus, Sengi Vidole-vinne au Isanje (Four-toed Elephant Shrew au Sengi)
- Rhynchocyon chrysopygus, Sengi au Njule wa Gedi (Golden-rumped Elephant Shrew au Sengi)
- Rhynchocyon cirnei, Sengi au Njule Madoa (Checkered Elephant Shrew au Sengi)
- Rhynchocyon petersi, Sengi au Njule Kinguja (Black and Rufous Elephant Shrew au Sengi)
- Rhynchocyon udzungwensis, Sengi au Njule wa Udzungwa (Grey-faced Elephant Shrew au Sengi)
- Rhynchocyon sp. nov., Sengi au Njule wa Boni (Boni Giant Sengi)
Picha[hariri | hariri chanzo]
- North african elephant shrew.jpg
Sengi kaskazi
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.