Nenda kwa yaliyomo

Sengi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Isanje)
Sengi
Isanje (Petrodromus tetradactylus)
Isanje (Petrodromus tetradactylus)
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota (Viumbe walio na seli zenye kiini)
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda ya juu: Afrotheria (Wanyama ambao wahenga wao waliishi Afrika)
Oda: Macroscelidea (Wanyama kama isanje)
Familia: Macroscelididae
Bonaparte, 1838
Ngazi za chini

Jenasi 4, spishi 20:

Sengi, njule au isanje ni wanyama wadogo wa familia Macroscelididae. Jina la njule litumika kwa jenasi Rhynchocyon na isanje litumika kwa Petrodromus tetradactylus. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara katika maeneo mbalimbali. Sifa bainifu mno ya sengi ni pua yao refu sana ambayo wanaweza kuipota ili kutafuta chakula. Hii inafanana kidogo na mwiro wa tembo na ni chimbuko cha jina lao la Kiingereza "elephant shrew". Miguu yao ni mirefu kwa kulinganisha na huenda wakirukaruka kama sungura. Rangi yao ni kahawia au kijivu kwa kawaida lakini spishi nyingine zina rangi kali pia kama nyekundu au njano. Hula invertebrata kama wadudu, buibui, majongoo, tandu na nyunguyungu.

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.