Sao Hill
Sao Hill ni kata ya mji wa Mafinga katika Mkoa wa Iringa, Tanzania, yenye Postikodi namba 51402.
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 3,799 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,765 waishio humo.[2]
Sao Hill ina umbali wa kilomita 15 kutoka Mafinga mjini kando ya barabara ya TANZAM kuelekea kusini (Mbeya).
Kitovu cha Sao hill ni kiwanda cha kusaga mbao maana Sao Hill iko katikati ya misitu mikubwa ya kupandwa hasa ya miti ya misonobari na mikalatusi. Misitu hiyo ilianzishwa zamani za ukoloni na siku hizi zinashughulukiwa na kampuni ya Kinorwei ya Green Resources.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kata za Wilaya ya Mafinga - Mkoa wa Iringa - Tanzania | ||
---|---|---|
Boma | Bumilayinga | Changarawe | Isalavanu | Kinyanambo | Rungemba | Sao Hill | Upendo | Wambi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Sao Hill kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |