Nenda kwa yaliyomo

Hifadhi ya Salonga

Majiranukta: 2°S 21°E / 2°S 21°E / -2; 21
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Salonga National Park)

2°S 21°E / 2°S 21°E / -2; 21

Mto Lulilaka ukipita Hifadhi ya Salonga
Bonobo wako kati ya viumbe vinavyohifadhiw katika Salonga

Hifadhi ya Salonga ni eneo la hifadhi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliopo katika beseni ya Mto Kongo . Ni hifadhi kubwa zaidi ya msitu wa mvua barani Afrika ikiwa na eneo la km² 36,000. Inaenea katika mikoa ya Mai-Ndombe, Equateur, Kasaï na Sankuru .

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Hifadhi hiyo iko katika eneo la misitu ya mvua asilia katikati ya mji mkuu Kinshasa na Kisangani. Hakuna barabara na sehemu kubwa ya hifadhi hiyo inaweza kutembelewa kwa njia ya mto pekee. Sehemu za kusini za hifadhi inakaliwa na Waiyaelima ambao wanaendelea maisha ya kuvinda na kulima wakitazamiwa wanatunza mazingira vema; hasa hawavindi bonobo.

Hifadhi ya Kitaifa ya Salonga ilianzishwa mnamo 1956 ikapata mipaka yake ya sasa kenye mwaka 1970 kwa amri ya rais Mobutu Sese Seko. Iliandikishwa na UNESCO katika orodha ya Urithi wa Dunia mwaka 1984. [1] Kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nusu mashariki ya nchi, iliongezwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia Hatarini mnamo 1999.

Wanyama katika hifadhi hiyo ni pamoja na Bonobo[2]. Kuna pia ndege wengi. [3]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Hopson, Mark (2011). "The Wilderness Myth: How the Failure of the American National Park Model Threatens the Survival of the Iyaelima Tribe and the Bonobo Chimpanzee". Earth Jurisprudence and Environmental Justice Journal. 1 (1).
  2. Falk, John (2008). "Why the Bonobos Need a Radio and Other (Unlikely) Lessons From Deepest Congo". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-03.
  3. "Salonga National Park". UNESCO. Iliwekwa mnamo 2013-12-14.
Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Salonga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.