Buibui-kofia
Buibui-kofia | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Aina ya buibui-kofia (Cryptocellus goodnighti)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 3; spishi 11 katika Afrika:
|
Buibui-kofia (kutoka kwa Kiing. hooded tickspider) ni arithropodi wa familia Ricinoididae, familia ya pekee ya oda Ricinulei katika ngeli Arachnida. Jina lao linatoka kwa aina ya “kofia” ambayo wanaweza kutumia ili kufunika kichwa, mdomo na kelisera (chelicerae). Kwa kawaida buibui-kofia wana urefu wa mm 5-10 na wanafanana na utitiri. Wataalamu wengine wanafikiri kwamba wadudu hawa wana mnasaba na utitiri, lakini wengine wanafikiri kwamba wana mnasaba na oda ya zamani ya Trigonotarbida iliyokwisha sasa. Kefalotoraksi (cephalothorax) na fumbatio zimeungwa kwa pediseli (pedicel) nyembamba kwa umbo wa mrija kama kwa buibui. Lakini ukingo wa fumbatio unaingia katika kunjo la gamba (carapace). Wana miguu minane kama arakinida wengine lakini jozi ya pili ni mirefu kuliko mingine na hutumika kama vipapasio. Hawana macho lakini spishi za zamani zilikuwa nayo na spishi za kisasa bado zina sehemu za kuhisi nuru. Mwenendo wa buibui-kofia haujulikani sana lakini inaonekana kwamba hula arithropodi wadogo kuliko hawa wenyewe.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Ricinoides westermannii
- Ricinoides afzelii
- Ricinoides atewa
- Ricinoides crassipalpe
- Ricinoides feae
- Ricinoides hanseni
- Ricinoides karschii
- Ricinoides leonensis
- Ricinoides megahanseni
- Ricinoides olounoua
- Ricinoides sjostedtii