Nenda kwa yaliyomo

Restitutus wa Karthago

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Restitutus wa Karthago (alifariki 373 hivi) alikuwa askofu wa mji huo wa Tunisia ya leo kuanzia mwaka 352 hadi kufa kwake.

Alitetea imani sahihi dhidi ya Uario.

Augustino wa Hippo alitoa hotuba ya kumsifu, lakini imepotea, hivi hatuna habari za jinsi alivyokufa[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Agosti[2][3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.