Rembrandt
Rembrandt Harmenszoon van Rijn (15 Julai 1606 – 4 Oktoba 1669) alikuwa mchoraji mashuhuri nchini Uholanzi wakati wa karne ya 17.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa mjini Leyden kama mtoto wa tisa wa msagi Harmen Gerritszoon van Rijn na mke wake Cornelia Neeltgen Willemsdochter van Zuytbrouck.
Alianza kuchora akiwa bado mtoto na mwanafunzi. Baada ya kumaliza shule alianza masomo kwenye chuo kikuu cha Leyden lakini aliacha masomo, badala yake aliingia katika mafunzo kwa mchoraji Jacob van Swanenburgh mjini Leyden.
Tangu mwaka 1631 alihamia Amsterdam alipopata wateja wengi waliomwajiri kuchora picha zao. Huko mwaka 1634 alimwoa Saskia van Uylenberg akazaa naye watoto wanne, lakini ni mmoja tu aliyeishi na kufikia umri mkubwa.
Katika sanaa yake alipata umaarufu kutokana na umakini wa picha zake. Alijua kucheza na giza na mwanga na picha ya "Walinzi wa Usiku" ni mfano bora.
Picha
[hariri | hariri chanzo]Picha zake mwenyewe
[hariri | hariri chanzo]-
Rembrandt mnamo 1628 alipokuwa na miaka 22
-
Mwenyewe mnamo 1630
-
Rembrandt mnamo 1632 alipotafutwa na watu kwa picha zao
-
Picha ya mwenyewe kama mkabaila wa mashariki, 1634.
-
Picha ya mwenyewe akiinama ukutani, 1639
-
Picha ya mwenyewe mnamo 1655
-
Mnamo 1669, mwaka wa kifo chake
Picha nyingine
[hariri | hariri chanzo]-
Somo la anatomia la Dk Nicolaes Tulp, 1631
-
Mhubiri Johannes Witenbogaert, 1633
-
Mke wake Saskia kama "Flora", 1635
-
Samsoni aking'olewa macho, 1636
-
Sherehe ya Belshaza, 1636-8
-
Mashine ya kusaga, 1648
-
Misalaba mitatu - mnamo 1653
-
Jan Six, 1654. (Six alikuwa rafiki tajiri wa Rembrandt)
-
Mwana mpotevu arudi nyumbani, 1669 hivi
-
Suzana na wazee, 1634