Nenda kwa yaliyomo

Rekodi za Dunia za Guinness

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Guinness World Records  
Guiness2010.JPG
Mwandishi (wa){{{mwandishi}}}
ISBNISBN:

Guinness World Records (iliyojulikana hadi mwaka wa 2000 kama The Guinness Books of World Records na kwa matoleo yaliyotangulia Marekani, kama The Guinness Book of World Records), ni kitabu cha marejeleo kinachochapishwa kila mwaka na ni mkusanyo wa rekodi za dunia za mafanikio ya binadamu pamoja na maajabu ya ulimwengu asili. Kitabu chenyewe kinashikilia rekodi ya dunia kama mfululizo wa kitabu cha nakala iliyohifadhiwa kilicho na mauzo ya juu zaidi. [1] Pia ni mojawapo ya vitabu ambavyo huibiwa sana kutoka maktaba ya umma katika Marekani. [2]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 4 Mei 1951, Sir Hugh Beaver, akiwa mkurugenzi wa Guinness Breweries, [3] alienda kwenye mchezo wa kupiga risasi kule Kaskazini Slob, kando na mto Slaney katika County Wexford, Ireland. Alijihusisha kwenye mabishano kuhusu ni ndege yupi wa mwitu aliyekuwa wa kasi sana Ulaya. Jioni hiyo akiwa Castlebridge House, aligundua ilikuwa vigumu kuthibitisha katika vitabu vya marejeleo kama koshin golden plover alikuwa ndege wa mwituni wa kasi sana wa Ulaya ama sivyo. [4] [5]

Beaver alijua kwamba lazima kuna maswali mengine kadhaa ambayo hujadiliwa katika majumba ya starehe katika Uingereza na Ireland, lakini hapakuwa kitabu cha kutatua ubishi kuhusu umahiri. Aling'amua kuwa kitabu cha majibu kwa masuala ya aina hii kingekuwa maarufu.

Wazo la Beaver lilikuja likatimilika wakati mfanyakazi wa Guinness, Christopher Chataway alipendekeza wanafunzi mapacha Norris na Ross McWhirter, waliokuwa wakiendesha shirika la utafiti mjini London. Ndugu hawa walikandarasiwa kukusanya kile kilicho julikana kama The Guinness Book of Records mwezi Agosti 1954. Nakala elfu moja zilichapishwa na kupeanwa bure. [6]

Baada ya kuanzisha Guinness Book of Records kwenye mtaa 107 Fleet Street, toleo la kwanza la kitabu hiki kilichokuwa na kurasa 197 kilifunganishwa tarehe 27 Agosti 1955 na kikawa cha kwanza kwenye orodha ya mauzo ya vitabu bora nchini Uingereza hata kabla ya Krismasi. "Ilikuwa njia ya kuimarisha mauzo-haikuwa njia ya kuunda pesa ," alisema Beaver. Mwaka uliofuata, ilizinduliwa Marekani na kuuza nakala 70,000.

Baada ya kitabu kuwa maarufu bila kutarajia, toleo zaidi zilichapishwa. Hatimaye, ikafuata muundo wa marekebisho mara moja kila mwaka iliyochapishwa katika Oktoba sanjari na mauzo ya Krismasi. McWhirters waliendelea kuchapisha vitabu hivyo na vingine vya kuhusiana kwa miaka mingi. Ndugu hao walikuwa na kamusi kumbukumbu - kwenye makala ya TV ya Record Breakers, kuhusiana na kitabu hicho. Walijibu maswali kutoka kwa watoto kwenye mkusanyiko kuhusiana na rekodi mbalimbali za dunia na wangewapa kawaida majibu sahihi. McWhirter Ross aliuawa na Provisional Irish Republican Army mwaka 1975. [7] Kufuatia mauaji ya McWhirter, kipengele katika maonyesho ambapo maswali kuhusu rekodi za hapo mbeleni kotoka kwa watoto yalijibiwa kiliitwa "Norris on the Spot".

Guinness World Records Ltd iliundwa mwaka wa 1954 kuchapisha kitabu cha kwanza.

Sterling Publishing ilimiliki haki za kitabu cha Guinness katika miaka ya 1970 na chini ya uongozi wao, kitabu hiki kilipata umaarufu Marekani.

Kundi la uchapishaji lilimilikiwa na Guinness Brewery na hatimaye Diageo hadi 2001 liliponunuliwa na Gullane Entertainment. Gullane nayo ikanunuliwa na HiT Entertainment mwaka 2002. Mnamo mwaka wa 2006, Apax Partners ilinunua HiT na hatimaye kuuzwa Guinness World Records mapema mwaka 2008 kwa Jim Pattison Group, ambayo pia ni kampuni msingi ya Ripley Entertainment, ambayo ina leseni ya kuendesha Guinness World Records 'Attractions. Pamoja na ofisi mjini New York na Tokyo,makao makuu ya kimataifa ya Guinness World Records yamebaki mjini London, wakati vivutio vya kumbukumbu ipo katika makao makuu ya Ripley katika Orlando, Florida.

Baadhi ya majaribio ya rekodi za dunia ni ya kustajabisha zaidi kuliko mengine: Suresh Joachim, dakika chache baada ya kuvunja rekodi ya dunia ya kupiga pasi ya masaa 55 na dakika 5, katika Shoppers World, Brampton.

Makala ya hivi karibuni yamelenga rekodi za umahiri wa washindani binadamu. Mashindano yapo kwa viwango mbalimbali kutoka kwa yale dhahiri kama kuinua uzito hadi uturushaji wa yai kwa umbali ulio mrefu zaidi, au kwa muda mrefu iliotumika kucheza Theft Auto IV au idadi ya hot dogs ambazo zinaweza kuliwa katika dakika kumi, ingawa mashindano ya kula na kunywa bia na pombe hayakubaliki tena pengine kwa hofu ya kuyahalalisha. Licha ya rekodi za mashindano, kuna habari za ukweli kama uvimbe mzito sana,mmea wa sumu zaidi, mto mfupi sana (Mto Roe), mchezo wa kuigiza unaochukuwa muda mwingi sana (Guiding Light) katika Marekani, wahusika waliodumu sana katika mchezo wa kuigiza (William Roache kwa Coronation Street nchini Uingereza, Ray Meagher kwa Home and Away muda mrefu zaidi (As the World Turns) katika Marekani, na mfanyabiashara maarufu sana duniani (Joe Girard), na zinginezo. Rekodi nyingi pia zinahusiana na binadamu mwenye umri mdogo kutimilisha kitu kama binadamu mwenye umri mdogo kutembelea mataifa yote ya ulimwengu akiwa Maurizio Giuliano. [8]

Kila toleo lina uteuzi wa rekodi nyingi katika mfumo habari wa Guinness, na vigezo vwa kuchagua vimebadilika na miaka iliyopita. Rekodi mpya huongezwa na rekodi ambazo zimevunjiliwa hoongezwa pia.

Kutolewa kwa Norris McWhirter kutoka jukumu la kuwa mshauri mwaka wa 1995 na baadaye maamuzi ya Diageo Plc kuuza Guinness World Records imeibadilisha kotoka muundo wake wa kuwa kama kitabu cha marejeleo, hadi kuwa mfano wa bidhaa. Mabadiliko haya yana maana kwamba rekodi nyingi za dunia zizijaorodheshwa katika kitabu (au kwenye tovuti), na zinaweza tu kujulikana kwa kuandika ombi kwa Guinness la kutaka 'kuvunja' rekodi. Kwa wale wasioweza kungojae muda wa hadi wiki 4-6 kwa majibu, Guinness itashughulikia maombi yao kwa dharura kwa kiwango cha pauni 300 (~dola 600).

Guinness Book of Records ni kitabu cha nakala iliyohifadhiwa kuuzwa zaidi duniani na hivyo kupata kuingia ndani kwenye kurasa zake. Vitabu kadhaa na filamu za televisheni pia zimetolewa. Msisitizo tena katika maonnyesho haya imekuwa kuvutia na kuburudisha kuliko kujulisha au kuelimisha.

Guinness World Records haifuatilia kipengee cha "Person with the most records" kwani hii hubadilika kila mara, na rekodi zingine zilizokuwepo huwenda sasa 'zilipumzishwa' na hivyo kipengee hiki kisingekuwa na usawa.

Mwaka 2005, Guinness iliteua 9 Novemba kama International Guinness World Records Day ili kuhimiza kuvunja rekodi za dunia na ilifafanuliwa kuwa "mafanikio zaidi". Toleo la mwaka wa 2006 lilibatizwa "tukio kubwa la kimataifa duniani," kwa wastani wa watu 100,000 kushiriki katika nchi 10. Utangazaji huu umeipa Guinness rekodi 2244 mpya zote zilizo halali katika miezi 12, ambayo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 173 kutoka mwaka uliopita. [9]

Mnamo Februari 2008, NBC ilionyesha The Top 100 Guinness World Records of All Time na Guinness World Records ilizirodhesha kwenye tovuti yao. [10]

Masuala ya maadili na usalama

[hariri | hariri chanzo]

Rekodi kadhaa za Ulimwengu zilizokuwa katika kitabu zimeondolewa kwa sababu za kimaadili. Kwa kuchapisha rekodi za ulimwengu kitengo, kitabu kinaweza kuwatia moyo wengine kujaribu kuvunja rekodi hizi hata kwa gharama ya afya na usalama wao. Kwa mfano, kufuatia uchapishaji wa rekodi wa "heaviest cat" , wamiliki wengi paka waliwalisha kupita kiwango cha afya njema na kwa hivyo,vipenge kama hivi viliondolewa. [11] Guinness Book pia iliondoa rekodi kwenye kitengo cha "eating and drinking records" kwa Mafanikio ya Binadamu mwaka 1991 kwa wasiwasi ya kwamba washindani wangeweza kudhuru na kumweka mchapishaji kwenye kesi za koti. Mabadiliko haya ni pamoja na kuondolewa kwa rekodi ya kunywa pombe, mvinyo na bia, pamoja na rekodi nyingine zisizo za kawaida kama vile kula vitu visivyo vya kawaida kama vile baiskeli na miti. [12] Rekodi nyingine kama vile kumeza upanga na uendeshaji wa magari (kwenye barabara za umma), zilifungiwa kwani washikiliaji wa rekodi hizi walizidisha kiwango kinacho dhaniwa salama kwa binadamu.

Kumekuwa na matukio ya rekodi zilizofungwa kufunguliwa. Kwa mfano,rekodi ya kumeza upanga iliorodheshwa kama iliyofungwa kwenye Guinness Book of World Records mwaka wa 1990, lakini kipindi cha elevishani cha Guinness World Records Primetime, kilichoanza mwaka 1998,kilikubalia ushindani wa watu tatu wa kumeza upanga (na vivyo toleo la 2007 Guinness World Records, kilichoanza mwaka 1998, kilikubalia ushindani wa watu tatu wa kumeza upanga (na vivyo toleo la 2007 Guinness World Records'' na kuendelea).

Mkururo wa barua pia hairuhusiwi. "Guinness World Records haikubali rekodi yoyote inayohusiana na mkurur wao barua, zilizotumwa posta au barua pepe. Ukipokea barua au barua pepe ambayo iliyo na ahadi ya kuchapisha majina ya wale wote wanaoendeleza kuituma, tafadhali iharibu, ni ukora. Hata ikidai kuhusika kwa Guinness World Records na huduma za posta, hawausiki. [13]

Majumba ya kumbukumbu

[hariri | hariri chanzo]
Jumba la Kumbukumbu la Guinness , Los Angeles, California.

Mnamo mwaka wa 1976, jumba la kumbukumbu la Guinness Book of World Records lilifunguliwa katika Empire State Building. Mlenga shabaha Bob Munden kisha akaenda ziara kutangaza Guinness World Records kwa kupiga risasi kutoka bastola aina ya single-action katika muda wa sekunde 1. [14] Miongoni mwa maonyesho kulikuwepo na sanamu ya mtu mrefu zaidi duniani, Robert Wadlow na mnyo wa ardhini mkubwa duniani , picha ya X-ray ya mmeza upanga ,kofia ya mhasiriwa wa kupigwa na umeme mara kadhaa Roy Sullivan ikiwemo na mashimo na viatu vya golf vilivyo rembeshwa vilivyouzwa kwa $ 6500. [15] Jumba hili lilifungwa.

Katika miaka ya hivi karibuni, kampuni ya Guinness imeruhusu kuweko kwa majumba ya kumbukumbu madogo maonyesho yakiwa kwa misingi ya kitabu hiki, kwa sasa (kama wa 2008) ziko katika miji maarufu kwa watalii: Tokyo, Copenhagen, San Antonio, Niagara Falls, Hollywood na Gatlinburg, Tennessee, pamoja na eneo mpya iliyopangwa kufungua katika Bangalore, India mwezi Februari 2010.

Wakati mmoja, kulikuwa na majumba ya kumbukumbu na maonyesho ya Guinness World Records katika Trocadero mjini London, Surfers Paradise, San Francisco, Orlando, Florida, [16] Atlantic City, New Jersey, [17] Las Vegas, Nevada [18] na San Antonio, Texas [17] lakini maeneo haya yalifungwa. Jumba la kumbukumbu la Orlando, lililofungwa mwaka 2002, lilibandikwa The Guinness Records Experience; [16] majumba ya Hollywood , Niagara Falls, Copenhagen, Gaitlinburg na, Tennessee awali pia yalibandikwa hivyo. [18]

Ingawa baadhi ya maonyesho ni ya kusisimua, kama sanamu ya mtu mrefu sana au mfupi sana duniani, au video za rekodi zikivunjwa, habari nyingi huonyeshwa kwa njia ya maandishi na picha tu.

Filamu za televisheni

[hariri | hariri chanzo]

Guinness World Records ina filamu za televisheni mbalimbali zinazoonyesha majaribio ya kuvunja rekodi za dunia, zikiwemo:

  • Guinness World Records UK
  • Guinness World Records Primetime
  • The Guinness Game
  • Australia's Guinness World Records
  • Guinness World Records: 50 Years, 50 Records
  • Ultimate Guinness World Records
  • Lo show dei record (Italian version)
  • Spain: El show de los récords (Antena 3) and Guinness World Records (Telecinco)
  • Record Breakers (BBC TV)
  • Guinness World Records Smashed - UK - Sky1 (Desemba)
  • Guinness World Records Portugal - PT - Sic
  • NZ Smashes Guinness World Records
  • Światowe Rekordy Guinnessa 2009 (Guinness World Records 2009) - Polen - Polsat

Kwa umaarufu wa televisheni halisia, GWR ilianza kujitangaza kama muanzilisha wa kitengo hiki, kwa misemo kama vile 'sisi tuliandika kitabu juu ya Reality TV'.

Ndugu wa McWhirter kwa pamoja na Roy Castle walituletea kipindi kwenye televisheni ya BBC, Record Breakers na kuanzia 1972 hadi kifo cha Ross mwaka 1975; Norris aliendelea kuonekana kwenye kipindi mpaka kustaafu kwake mwaka wa 1994.

Toleo la michezo

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka wa 2008, Guinness World Records ilizindua toleo lake la Gamer's edition kwa muungano na Twin Galaxies. Gamer's Edition ina kurasa 258, zaidi ya rekodi 1236 za dunia kuhusiana michezo ya video na mahojiano manne ikiwemo ile na nmwanzilishi wa Twin Galaxies, Walter Day.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Ashrita Furman of Queens, New York, the individual who holds the record for setting the most Guinness World Records [35]
  • Herostratic fame, named after Herostratus, who destroyed the Temple of Artemis for the single reason of having his name immortalized in history.
  • Limca Book of Records, a record book of Indian origin.
  • [36], A video game based on the book.
  1. Watson, Bruce. (Agust 2005). "World's Unlikeliest Bestseller". Smithsonian, uk. 76-81.
  2. "Book deals for a steal", 4 Mei 2008, The Times (South Africa), Retrieved 2009-10-29
  3. Guinness Book of Records collectors' web-site
  4. Early history of Guinness World Records, p. 2
  5. Richard Cavendish. "Publication of the Guinness Book of Records: 27 Agosti 1955". 
  6. "History of Guinness Book of Records". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-05-13. Iliwekwa mnamo 2007-04-29.
  7. "Norris McWhirter Dies; 'Guinness Book' Co-Founder". The Washington Post. 21 Aprili 2004. Iliwekwa mnamo 2009-09-29.
  8. Guinness Book of World Records 2006, page 126 of UK edition.
  9. "Records Shatter Across the Globe in Honor of Guinness World Records Day 2006". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-18. Iliwekwa mnamo 2007-04-29.
  10. Guinness World Records Live: Top 100. Guinness World Records. Retrieved on 6 Novemba 2008.
  11. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-19. Iliwekwa mnamo 2009-12-09.
  12. Guinness Book of World Records 1990 edition, s. 464
  13. Guinness World Records - Break A Record - Frequently Asked Questions (FAQ)
  14. Bob Munden - Munden Enterprises, Fast Draw, Six-Gun Magic, Custom Gun Work, shooting videos, dvds, School of the Fast Gun, history of fast draw, appearances
  15. In Praise of Facts, by John Leonard, the introduction to the New York Times Desk Reference
  16. 16.0 16.1 Brown, Robert H. "The Guinness World Records Experience: one of Florida's Lost Tourist Attractions". Iliwekwa mnamo 2009-02-01.
  17. 17.0 17.1 Ripley Entertainment, Inc. "Guinness World Records Experience locations". Iliwekwa mnamo 2009-02-01.
  18. 18.0 18.1 Ripley Entertainment, Inc. (2002-11-20). "Guinness World Records Experience locations". Internet Archive Wayback Machine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2002-11-20. Iliwekwa mnamo 2009-02-01.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  • Guinness World Attractions (the official Museums website)
  • Guinness World Records ( the official Book website)
  • The Jim Pattison Group (parent company)