Rebeka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Spagnoletto: Yakobo akiibia baraka ya Isaka kwa msaada wa Rebeka (1637), Prado, Madrid (Hispania).
Spagnoletto: Yakobo akiibia baraka ya Isaka kwa msaada wa Rebeka (1637), Prado, Madrid (Hispania).

Rebeka (kwa Kiebrania רבקה, Rivqah) alikuwa binamu na mke wa Isaka ambaye, baada ya utasa wa muda mrefu, hatimaye alimzalia watoto pacha Esau (au Edomu, babu wa Waedomu) na Yakobo Israeli (babu wa Waisraeli).

Kwa ujanja wake alifaulu kumfanya mume wake atoe baraka iliyokuwa haki ya mtoto wa kwanza kwa mdogo wake.

Anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Septemba.

Habari katika Biblia[hariri | hariri chanzo]

Kadiri ya Mwa 25:19-34, Rebeka alimzalia Isaka watoto pacha wenye sura na silika tofauti, Esau na Yakobo. Wa kwanza analaumiwa hasa kwa kupuuzia baraka ya Mungu iliyokuwa haki ya kifunguamimba: kwa sahani ya dengu alikubali kukosa neema zile zote alizojitwalia Yakobo kwa imani yake (Eb 12:16-17).

Mwa 27 inasimulia jinsi Yakobo, akifundishwa na mama yake, alivyoweza kubarikiwa na baba. Ingawa uongo wake haukubaliki (Hos 12:3-5), Mungu alithibitisha baraka ya Isaka kadiri ya desturi yake ya kumpendelea mdogo: hivyo Yakobo, aliyekimbia nchi yake ana fimbo tu, alirudi miaka ishirini baadaye ana wake 2, masuria 2, watoto 11 na mifugo wengi ajabu (Mwa 32). Kabla hajaingia nchi yake Mungu alishindana naye usiku kucha akalazimika kumbariki na kumtajia jina jipya, Israeli.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rebeka kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.