Queen Sendiga
Queen Sendiga | |
---|---|
Amezaliwa | 1973 |
Utaifa | Mtanzania |
Majina mengine | Queen Cuthbert Sendiga |
Kazi yake | Mwanasiasa, Mwanaharakati, Mfanyabiashara, Mkuu wa Mkoa wa Manyara |
Chama cha siasa | Alliance for Democratic Change |
Mwenza | Maneno Mbegu (m. 2013–present) |
Watoto | 3 |
Queen Cuthbert Sendiga (amezaliwa Rondo, mkoa wa Lindi 1973) ni mwanasiasa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa tangu Mei, 2021. Pia ni mwanaharakati na mfanyabiashara nchini Tanzania.
Ni Naibu Katibu Taifa wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC). Mwaka 2020, Queen aliwahi kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho. [1]
Maisha yake
[hariri | hariri chanzo]Queen Sendiga ni mkazi wa mkoa wa Dar es Salaam.
Kazi zake
[hariri | hariri chanzo]Queen katika siasa alikuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM mpaka mwaka 2014 alipoamua kuhama na kujiunga na chama cha Alliance for Democratic Change (ADC). Mwaka 2015 kwenye uchaguzi mkuu Tanzania aliwania nafasi ya ubunge jimbo la Kawe kupitika chama cha ADC ila hakufanikiwa kushinda.
Mwaka 2020 kwenye chaguzi za Tanzania alichaguliwa na chama chake cha ADC kuwania nafasi ya urais Tanzania, wakiwa wanawake wawili kupitia vyama vya upinzani na Cecilia Mwanga wa chama cha Demokrasia Makini [2] [3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Queen Sendiga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |