Puducherry

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fukwe ya bandari ya Puducherry
Maeneo ya Pondicherry nchini Uhindi
Ubao wenye jina la mtaa kwa Kifaransa na Kitamili

Puducherry (inayojulikana kimataifa zaidi kama Pondicherry kama ilivyokuwa hadi mwaka 2006) ni eneo maalumu la kitaifa nchini Uhindi. Ndani yake kuna maeneo madogo manne ya pekee yanayohesabiwa kwa pamoja kama eneo la kitaifa au Union Territory.

Hizo sehemu nne ni Pondicherry, Karaikal, Yanam na Mahé. Yalikuwa makoloni madogo ya Ufaransa katika Uhindi kusini, yaliyokaa pekee na Uhindi wa Kiingereza, yakakabidhiwa na Ufaransa kwa Uhindi huru mwaka 1962. Kimsingi kila sehemu ni mji mdogo wa pwani pamoja na mazingira kidogo karibu nao.

Jumla ya maeneo yote ni km² 492; kati ya sehemu nne Pondicherry (km² 290) na Karaikal (km² 160) zimezungukwa na eneo la jimbo la Tamil Nadu; Yanam (km² 20) liko ndani ya eneo la jimbo la Andhra Pradesh na Mahé (km² 9) imezungukwa na jimbo la Kerala.

Wakazi wote ni 1,244,464 (2011).

Lugha rasmi za Puducherry zinategemea lugha kuu ya mazingira ya kila sehemu: kwa Pondicherry na Karakal ni Kitamil, kwa Yanam ni Kitelugu na kwa Mahe ni Kimalayalam. Kifaransa bado ni lugha rasmi lakini haitumiki sana: hali halisi serikali inafanya kazi kwa kutumia Kiingereza.

Makala hii kuhusu maeneo ya Uhindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Puducherry kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.