Mahé

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ufukoni wa Mahé

Mahé ni kisiwa kikubwa cha funguvisiwa vya Shelisheli. Urefu wake ni 28 km na upana wake 8 km. Eneo lake ni 154,7 km².

Mahe ina wakazi 72,000 ambao ni sawa na asilimia 90 za wakazi wote wa Shelisheli.

Mji mkubwa ni Victoria ambayo ni pia mji mkuu wa taifa la Shelisheli.

Biashara kuu ya Mahe ni utalii. Karibu watalii wote wanaotembelea visiwa wanapita kwenye uwanja wa ndege wa Victoria.

Bandari ya Victoria

Sehemu kubwa za Mahe zimefunikwa na misitu minene. Mlima mkubwa ni Morne Seychellois mwenye kimo cha mita 905 juu ya UB.

Kisiwa kilitembelewa na Waingereza mnmo mwaka 1609 na wakati ule haukuwa na wakazi. Wafaransa waliunda makazi ya kwanza ya kudumu mnamo 1742 wakaanzisha mashamba na kuchukua wafungwa kama watumwa waliolima mashamba haya. 1814 Mahe pamoja na funguvisiwa ilitwaliwa na Uingereza na kuwa koloni yake hadi uhuru wa nchi mwaka 1976.