Nenda kwa yaliyomo

Prudencia Paul Kimiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Prudencia Paul Kimiti
Amezaliwa1978
UtaifaMtanzania
Majina menginePrudencia Paul Orridge MBE
Kazi yakeni mkuu wa kitengo cha upelelezi

Prudencia Paul Orridge MBE (alizaliwa mkoa wa Rukwa, mwaka 1978) ni Mtanzania aliye kuwa mkuu wa kitengo cha forodha katika idara ya Huduma za upelelezi wa tuhuma za udanganyifu katika kulipa kodi ya Taasisi ya mapato na forodha nchini Uingereza, lakini pia akitumia muda wake mwingi kama mwanaharakati wa haki za watu weusi..

Huduma za Upelelezi wa Tuhuma za Udanganyifu katika Kulipa Kodi ya Taasisi ya Mapato na Forodha ya Uingereza ni Idara maalum ndani ya serikali ya Uingereza yenye jukumu la kuchunguza na kupambana na aina mbalimbali za udanganyifu na uhalifu wa kifedha.

Prudencia, mtoto wa tatu wa waziri wa zamani Paul Peter Kimiti, amekabidhiwa tuzo ya heshima na Princess Anne, binti pekee wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza na dada pekee wa Mfalme Charles III.

April 23, 2022 alijulishwa na alikuwa waziri mkuu wa Uingereza wakati huo Boris Johson kuwa, jina lake limechomoza miongoni mwa majina ya kuwa watu wachache katakao tunukiwa tuzo ya heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika masuala ya jamii hasa watu weusi na watu wanaotaka bara la Asia waishio nchini Uingereza. kwa utamaduni uliyozoeleka nchini Uingereza, malkia alikuwa akitoa tuzo mara mbili kwa mwaka kwa watu wa kawaida wanaofanya vizuri katika jamii katika siku ya mwaka mpya, lakini pia tuzo zingine zikuwa zikitolewa alipokuwa anasheherekea siku ya kuzaliwa.

wachambuzi wa masuala mbalimbali za kimataifa wanasema huo ulikuwa ni utaratibu aliokuwa amejiwekea wakati wa enzi za uhai lakini inavyoonekana kwa asilimia kubwa inaweza kufutwa na mrithi wake ambaye ni Mfalme Charles III.

Tuzo hiyo ilitokana na jina lake kupendekezwa na wafanyakazi wenzake, kisha jina hilo lilipitishwa na kamati maalum, hatimaye ilipelekwa kwa waziri mkuu wa uingereza kabla ya kupelekwa kwa Malkia Elizabeth ll wakati huo kabla ya kifo chake September 8, 2022.

katika kutimiza azma ya malkia Elizabeth aliyokuwa nayo kabla ya kifo, mtoto wa pili wa malkia Elizabeth ll na ni dada wa pekee wa Mfalme charlrs lll ambaye ametunuku tuzo hiyo ya heshima katika eneo maalumu ya Windsor Castle huko akishuhudiwa na watu mbalimabli wakiwemo waziri wake mzee Paul Kimiti na mkwewe.

Mwaka 2020 binti huyo wa kitanzania, alikuwa miongoni mwa watu watatu waliochaguliwa kutembelea mataifa matatu barani Afrika ikiwemo Tanzania, Madagaska na Namibia katika kuwafundisha maafisa wa TRA namna sahihi na bora zaidi ya kuthamini bidhaa zinazoingia kutoka nchi nyingine. Baada ya kutunukiwa Tuzo hiyo, Prudencia amesema hii itakuwa historia katika maisha yake yote tuzo hiyo ni heshima kubwa sana kwangu binafsi, kwa Familia, na kwa Watanzania wote, akijisikia fahari na mtu mwenye bahati baada ya mchango wake katika jamii kutambuliwa na kupewa heshima kubwa na malkia Elizabeth II enzi za uhai wake.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Prudencia Paul Kimiti kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.