Nenda kwa yaliyomo

Protase Rugambwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Protase Rugambwa

Protase Rugambwa (alizaliwa Bunena, mkoa wa Kagera, 31 Mei 1960) ni askofu mkuu wa jimbo kuu la Tabora nchini Tanzania aliyeteuliwa kuwa kardinali wa tatu wa Kanisa Katoliki kutoka nchi hiyo.

Baada ya masomo yake, alipewa upadrisho na Papa Yohane Paulo II huko Dar es Salaam tarehe 2 Septemba 1990.

Miaka 1994-1998 alisomea Roma hadi kupata PhD katika teolojia ya uchungaji.

Baada ya kurudi Tanzania, mwaka 2002 aliitwa Roma kufanya kazi katika ofisi ya Idara ya Uinjilishaji wa Mataifa hadi mwaka 2008, ambapo tarehe 18 Januari Papa Benedikto XVI alimteua kuwa askofu wa jimbo la Kigoma ambalo aliliongoza hadi mwaka 2012 alipoitwa tena Roma kuwa Katibu Msaidiki, halafu Katibu wa idara hiyohiyo ya Papa.

Mnamo Aprili 2023 aliteuliwa na Papa Fransisko kuwa askofu mwandamizi wa Jimbo Kuu la Tabora.

Tarehe 30 Septemba 2023 Papa huyohuyo alimteua kuwa kardinali na tarehe 10 Novemba 2023 akamrithi Paul R. Ruzoka kama askofu mkuu wa Tabora.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.