Potito wa Sardica

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Potito iliyochongwa na Paolo Guidotti, kanisa kuu la Pisa.

Potito wa Sardica (alifariki Sardica, leo Sofia, Bulgaria, 160 hivi[1]) alikuwa mvulana wa mji huo aliyeongokea Ukristo na kufia dini yake hiyo hukohuko kwa kuchomwa kwa upanga baada ya mateso mengi wakati wa dhuluma ya kaisari Antoninus Pius.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Januari[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.