Upinde wa mvua
Upinde wa mvua (kwa Kiingereza "rainbow") ni tao la rangi mbalimbali angani ambalo linaweza kuonekana wakati Jua huangaza kupitia matone ya mvua inayoanguka.
Mfano wa rangi hizo huanza na nyekundu nje na hubadilika kupitia rangi ya chungwa, njano, kijani, bluu, na urujuani ndani. Rangi hizi na ufuatano ni sehemu ya spektra ya nuru.
Upinde wa mvua huundwa wakati mwanga unapindwa ukiingia matone ya maji hewani, unagawanyika kuwa rangi tofauti, na kurudishwa nyuma. Hapa spektra ya nuru inaonekana ambayo ni rangi mbalimbali zinazopatikana ndani ya mwanga ambayo sisi tunaona kwa macho kama nyeupe tu.
Upinde wa mvua upo katika umbo la duara. Chini, sehemu ya chini imefichwa, lakini angani, kama ndege ya kuruka, inaweza kuonekana kama mviringo karibu na eneo la kinyume na jua.
Mara nyingi upinde wa mvua huonekana baada ya dhoruba, na ni alama maarufu ya amani na maelewano kati ya watu wa tamaduni nyingi.
Sababu
Athari ya upinde wa mvua inaweza kuonekana wakati:
- Kuna matone ya maji katika hewa; na
- Jua linatoa mwanga nyuma ya mwangaliaji kwa umbali wa chini au pembe.
Upinde wa mvua daima huonekana kinyume na jua: huunda duru karibu na kivuli cha kichwa chako (ambayo ni hatua kinyume na jua).
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Upinde wa mvua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |