Kuchamsitu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Phylloscopidae)
Kuchamsitu
Kuchamsitu koo-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Phylloscopidae (Ndege walio na mnasaba na kuchamsitu)
Alström, Ericson, Olsson & Sundberg, 2006
Ngazi za chini

Jenasi 2; spishi 16 katika Afrika:

Kuchamsitu ni ndege wadogo wa familia Phylloscopidae. Wanafanana na shoro, kucha na kuchanyika, na zamani wote waliainishwa pamoja katika familia Sylviidae. Spishi za Phylloscopus zina rangi ya kahawia au kijani mgongoni na nyeupe au njano chini. Zile za Seicercus zina rangi kali zaidi, kijani mgongoni na njano chini; zina milia kichwani na mviringo wa jicho mweupe au njano. Ndege hawa wanatokea misitu ya Afrika, Asia na Ulaya. Spishi zinazozaa katika kanda za halijoto ya wastani huhamia kusi, zile za Ulaya huenda Afrika. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo la kikombe ndani ya uoto mzito, mara nyingi karibu na ardhi. Jike huyataga mayai 2-7.

Spishi za Afrika (na Ulaya)[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]