Kuchanyika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kuchanyika
Kuchanyika wa Ulaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Cettiidae (Ndege walio na mnasaba na kuchanyika)
Jenasi: Abroscopus E.C.S. Baker, 1930

Cettia Bonaparte, 1834
Eremomela Sundevall, 1850
Erythrocercus Hartlaub, 1857
Graueria Hartert, 1908
Hemitesia Chapin, 1948
Horornis Hodgson, 1845
Hylia Cassin, 1859
Pholidornis Hartlaub, 1857
Phyllergates Sharpe, 1883
Tesia Hodgson, 1837
Tickellia Blyth, 1861
Urosphena Swinhoe, 1977

Kuchanyika ni ndege wadogo wa familia Cettiidae. Spishi za Erythrocercus zinaitwa ndwindwi au dwidwi. Ndege hawa wanafanana na shoro, kucha na kuchamsitu, na zamani wote waliainishwa pamoja katika familia Sylviidae. Spishi nyingine za kuchanyika zina mkia mrefu, nyingine zina mkia mfupi sana. Zina rangi ya kahawia au kijivu mgongoni na nyeupe au njano chini; spishi kadhaa zina rangi kali (Tesia k.m.). Spishi za Cettia tu zinatokea Ulaya, nyingine zinatokea misitu ya Afrika na Asia. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa kigoga, nyuzinyuzi, mizizi na/au majani. Jike huyataga mayai 2-6.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]