Nenda kwa yaliyomo

Shoro (Cettiidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Cettiidae)
Shoro
Shoro wa Cetti
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Cettiidae (Ndege walio na mnasaba na kuchanyika)
Alström, Ericson, Olsson & Sundberg, 2006
Ngazi za chini

Jenasi 7, spishi 2 katika Afrika:

Shoro ni ndege wadogo wa familia Cettiidae. Spishi za familia Acrocephalidae na Locustellidae huitwa shoro pia na wanafanana. Zina rangi ya kahawia au kijivu mgongoni na nyeupe au njano chini; spishi kadhaa zina rangi kali (Tesia k.m.). Shoro wa Cetti (Cettia cetti) anatokea Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Shoro mkia-mfupi anatokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa kigoga, nyuzinyuzi, mizizi na/au majani. Jike huyataga mayai 2-6.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]