Kucha (Sylviidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sylviidae)
Kucha
Kucha utosi-mweusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Sylviidae (Ndege walio na mnasaba na kucha)
Ngazi za chini

Jenasi 20:

Kucha ni ndege wadogo wa familia Sylviidae. Wanafanana na shoro, kuchanyika na kuchamsitu, na zamani wote waliainishwa pamoja katika Sylviidae. Zamani kucha wa Afrika kusini kwa Sahara waliainishwa katika jenasi Parisoma lakini sasa wamewekwa katika jenasi Sylvia. Pengine jenasi Conostoma, Paradoxornis na jenasi nyingine za madomo-kasuku ziainishwa katika familia Paradoxornithidae. Spishi nyingi za kucha huimba vizuri sana. Ndege hawa wana rangi ya kahawia au kijivu mgongoni na nyeupe chini. Spishi kadhaa zina rangi kali zaidi. Wanatokea kanda za halijoto ya wastani na za nusutropiki katika Afrika, Asia na Ulaya. Spishi nyingi za Sylvia za Ulaya na Asia huhamia Afrika kusini kwa Sahara wakati wa majira ya baridi. Kucha hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe ndani ya uoto mzito, mara nyingi karibu na ardhi. Jike huyataga mayai 3-7.

Spishi za Afrika (na Ulaya)[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]