Kuchanyika
Mandhari
(Elekezwa kutoka Pholidornis)
Kuchanyika | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Kuchanyika tumbo-njano
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Jenasi 2, i katika Afrika:
|
Kuchanyika ni ndege wadogo wa nusufamilia Eremomelinae katika familia Cisticolidae. Ndege hawa wanafanana na videnenda, lakini hawana michirizi kama hao na mara nyingi wana rangi ya manjano kwenye sehemu mbalimbali za mwili. Spishi za Eremomela zinatokea misitu ya Afrika na zile za Micromacronus huko Asia. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa kigoga, nyuzinyuzi, mizizi na/au majani. Jike huyataga mayai 2-6.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Eremomela atricollis, Kuchanyika Mkufu-mweusi (Black-necked Eremomela)
- Eremomela badiceps, Kuchanyika Utosi-mwekundu (Rufous-crowned Eremomela)
- Eremomela canescens, Kuchanyika Mgongo-kijani (Green-backed Eremomela)
- Eremomela flavicrissalis, Kuchanyika Tako-njano (Yellow-vented Eremomela)
- Eremomela gregalis, Kuchanyika wa Karuu (Karoo au Yellow-rumped Eremomela)
- Eremomela icteropygialis, Kuchanyika Tumbo-njano (Yellow-bellied Eremomela)
- Eremomela pusilla, Kuchanyika wa Senegali (Senegal Eremomela)
- Eremomela salvadorii, Kuchanyika wa Salvadori (Salvadori's Eremomela)
- Eremomela scotops, Kuchanyika Utosi-kijani (Green-capped Eremomela)
- Eremomela turneri, Kuchanyika Paji-jekundu (Turner's Eremomela)
- Eremomela usticollis, Kuchanyika kahawiachekundu (Burnt-necked Eremomela)
Spishi za Asia
[hariri | hariri chanzo]- Micromacronus leytensis (Visayan miniature babbler)
- Micromacronus sordidus (Mindanao miniature babbler)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kuchanyika mkufu-mweusi
-
Kuchabyika utosi-mwekundu
-
Kuchanyika tako-njano
-
Kuchanyika wa Karuu
-
Kuchanyika wa Senegali
-
Kuchanyika wa Salvadori
-
Kuchanyika utosi-kijani
-
Kuchanyika kahawiachekundu