Nenda kwa yaliyomo

Sungura wa Kizungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Oryctolagus)
Sungura wa Kizungu
Sungura wa Kizungu
Sungura wa Kizungu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Lagomorpha (Wanyama kama sungura)
Familia: Leporidae (Wanyama walio na mnasaba na sungura)
Jenasi: Oryctolagus
Spishi: O. cuniculus
(Linnaeus, 1758)

Sungura wa Kizungu ni mamalia wadogo waliomo katika familia ya Leporidae ya oda ya Lagomorpha na wanaopatikana sehemu mbalimbali za dunia. Katika familia ya sungura kuna jenasi kumi na moja. Pia kuna spishi nyingine za sungura na hizo pamoja na pika zinaunda oda ya Lagomorpha.

Mahali pa makazi[hariri | hariri chanzo]

Maingilio ya shimo la sungura na vinyesi nje karibu.

Asili ya sungura wa kizungu ni Ulaya ya magharibi-kusini (Hispania na Ureno) na Afrika ya magharibi-kaskazini (Maroko na Aljeria) lakini wamewasilishwa katika maeneo mengi duniani. Mara nyingi huleta hasara kubwa, k.m. katika Australia, Nyuzilandi na Hawaii. Sungura huishi sana kwenye maeneo yenye malisho ya majani, miti, misituni, vichakani na nyikani. Pia huweza kuishi jangwani na sehemu tepe – tepe.

Tabia na maumbo yao[hariri | hariri chanzo]

Masikio marefu ya sungura wa Kizungu, karibu sentimeta 10 pengine ni mahususi kwa ajili ya kutambua adui. Wana miguu ya nyuma yenye nguvu, kila mguu una vidole vitano, huku kidole kimoja kikiwa kidogo mno. Ukubwa wao ni takribani sm 20 mpaka 50 na uzito wa kilogramu 0.4 mpaka 2. Manyoya yao huwa marefu laini na rangi kati ya kahawia kijivu na manjano hafifu. Mkia wao huwa mfupi, uliojaa manyoya. [1]

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Sungura wakiwa wanyama wanaowindwa kwa ajili ya chakula huchunguza kwa makini kubwa makazi yao mapya na pindi na pindi wanapopata vitisho / hatari hutulia kimya na kutazama kwa makini. Uoni wa sungura ni uwanja mpana na kwa kiasi kikubwa huweza hata kuona juu ya vichwa vyao hata akiwa ndani sungura atatafiti hali ya anga.

Uzazi[hariri | hariri chanzo]

Sungura wa kufugwa, saa moja baada ya kuzaliwa.

Jike la sungura wa Kizungu huwa hawatoi mayai mpaka baada ya kupandwa. Uterasi yao imegawanyika sehemu mbili hivyo kupandana kunaweza kuhusisha matendo kadhaa ambayo yaweza kusababisha mimba kadhaa kutoka kwa madume tofauti. Dume la sungura huwa hawawezi kutoa shahawa wakati wa joto la kiangazi (majira ya joto). Sungura jike hubeba mimba kwa siku 30 mpaka 32 na kuzaa watoto 12 – 13. Wakati mwingine huweza kufikisha watoto 18.

Tundu na watoto.

Chakula na tabia za kula[hariri | hariri chanzo]

Sungura ni wanyama wala nyasi wanaokula hasa nyasi na majani ya magugu. Kwa bahati mbaya chakula chao huwa na kiai kikubwa cha selulozi ambayo ni kazi sana kumeng’enya. Sungura hutatua tatizo hili kwa kutoa aina mbili za kinyesi; kimoja huwa kigumu na kingine huwa kilaini na chenye kunata. Hiki cha pili laini na chenye kunata huliwa tena. Hivyo sungura hula vinyesi vyao badala ya kuwa kama ng’ombe na wanyamma wengine ambao hula baada ya kucheua ili kumeng’enywa ili kupata virutubisho zaidi. [2]

Sungura haraka sana kwa nusu saa ya kwanza ya malisho, maranyingi mchana karibu na jioni, ikifuatia nusu saa nyingine ambapo hula kwa kuchagua sana chakula. Ni wakati huu pia ndio sungura atatoa kinyesi kigumu kama uchafu, ambacho yeye hatakila. Kama mazingira hayahatarishi sungura atabaki nje kwa masaa mengi. Akiwa nje ya shimo lake sungura huwa akila kile jinyesi chake laini na hii huonwa mara chache zaidi, sababu hula tu baada ya kukitoa. Kwa kawaida sungura kinyesi chake kati ya saa mbili asubuhi na sa kumi na moja jioni akiwa ndani ya shimo lake.

Kinyesi kigumu na kikavu mara nyingi hutolewa nje ya shimo na kama inavyofahamika na kuliwa tena. Huku kile laini hutolewa ndani ya shimo saa chache baada ys kula wakati ambao pia kinyesi kikavu kishatolewa.

Kama wanyama wa kufugwa[hariri | hariri chanzo]

Sungura pindi wanapowekwa ndani ya nyumba kwa ajili ya kufugwa hutambulika kama sungura wa nyumbani. Wakiwa ndani ya nyumba sungura huwekwa kwenye sanduku lao kubwa lenye nafasi ya wao kutmbea – tembea. Huweza hata kuzoeshwa kutumia sanduku vingine kuweka uchafu au hata kuitikia kusogea pindi wanapoitwa. Pia huweza kuishi kama rafiki wa karibu kabisa na watu kwa kuwa kwenye sanduku linalioweza kufikia kirahisi. Popote walipo na maranyingi huwekwa sebuleni au vyumbani. Wakati wa mchana huweza kuwekwa mahali salama na wazi ili wapate mwanga wa jua na kurudishwa ndani giza linapoingia.

Wakiwa ndani hasa ya visanduku vyao sungura huwekewa malazi na wanasesere pia. Huongezewa nyingine kwa ajili ya mzoezi kama vile kuwekewa mandhari waliyopaswa kuwa nayo mwituni. Sungura huweza kuchangamana kwa urahisi hata na wanyama wengine. Huweza kuishi hata na mbwa, paka na wakati mwingine hata nungu bandia. Sungura hawafai sana watoto wadogo, sababu watoto wadogo wa binadamu huwa hawawezi kuwa watulivu kama vile sungura wanavyohitaji. Sungura wana mifupa laini sana migongono mwao na hutakiwa kushikiliwa tumboni mwao wakati wa kunyanyuliwa.

Kama chakula na mavazi[hariri | hariri chanzo]

Sungura wa Australia 'Rabbiter' circa 1900
Mzigo wa ngozi ya sungura, Northern Tablelands, New South Wales
Sungura huweza kuchinjwa kwa nyama na nyama yake kutumika

Sungura wa Kizungu ni chakula kwa watu wa Ulaya, Australia na Nyuzilandi. Sungura bado ni maarufu na wanauzwa katika bucha za huko Uingereza, japo si mara nyingi sana kwenye masoko makubwa. Sungura pia walikuwa wanauzwa sana huko Australia na tangu uzuke ugonjwa wa sungura huko watu waliacha tena kula nyama ya sungura. Wanapotumika kwa chakula sungura huwindwa kwa ajili ya nyama. Sungura huwindwa kwa bunduki, na wakati mwingine mbwa husaidia kuwinda. Maeneo mengine sungura hufugwa maalumu kwa ajili ya nyama. Sungura huuwawa kwa kugongwa kwa nguvu kisogoni kabla ya kuchinjwa. Nyama ya sungura ni chanzo kizuri cha protini. Inaweza kutumiwa kw namna nyingi ambavyo nyama ya kuku ingeweeza kutumika. Kuna baadhi ya wapishi husema nyama ya sungura huwa na radha ya kuku. Sungura pia ni chakula kizuri kwa chatu hasa kwa huko Bama ambapo chatu hula sungura mmoja kila baada ya wiki moja. Ngozi ya sungura ikiwa na manyoya, hutumika nguo na mavazi mbalimbali kama vile kofia. Sungura waitwao angora hufugwa kwa ajili ya nywele zao ndefu zxitumikazo kwa ajili ya nguo kama vile kondoo wa sufu. Sungura pia huzalisha mbolea nzuri, na mkojo wao wenye naitrojeni ya kutosha hufanya milimao izae vizuri sana. Maziwa ya sungura pia huwa dawa na kirutubisho kizuri sana kwasababu ya kiwango kikubwa cha protini.

Matatizo kwenye mazingira[hariri | hariri chanzo]

Sungura wamekuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira, pindi wanapowekwea kwenye mazingira mapya. Kutokana na namna ya kula,na kiwango chao kikubwa cha kuzaliana, sungura wa mwituni huwa chanzo kikubwa cha tatizo hasa kwenye kilimo. Njia mbalimbali zikiwemo kupiga risasi kuweka uzio, kunyunyiza dawa na kuweka mitego hujaribu kudhibiti wingi wao,lakini ike ya kuweka magonjwa yanayowahatarisha sungura tu ndio hufanikiwa sana. Mfano ugonjwa wa myxomatosis na calicivirus’ ambayo ni virusi waliotengenezwa kwa mara ya kwanza huko Hispania kuwasaidia wakulima kuwadhibiti sungura.

Tamaduni[hariri | hariri chanzo]

Sungura maranyingi hutumika kama alama ya uzazi au kuzaliwa tena na mara nyingi wakihusishwa na Pasaka na majira ya kuchipua. Na sungura kama mnyama anayewindwa tu (asiyewindwa) huwa alama nyingine ya pasaka, kama alama ya mnyama asiyekosa (asiyemdhambi). Zaidi sungura hutumika kama alama ya mfanya ngono hovyo, ambayo inahusiana na mtazamo wa binadamu wa kutokuwa na mdhambi na pia kama sifa yake ya uwezo mkubwa wa kuzaliana.