Opus Dei
Opus Dei au kwa jina kamili "Praelatura Sanctae Crucis et Opus Dei" (kwa Kilatini "Jimbo la Msalaba Mtakatifu na la Kazi ya Mungu") ni jimbo pekee la kimataifa (lisilo na eneo) ndani ya Kanisa Katoliki.
Shabaha yake ni kujenga maisha ya kidini kwenye ngazi ya familia na kuwasaidia waumini kuishi kitakatifu kwa kulingana na masharti ya imani na maadili ya Ukristo kufuatana na mafundisho ya kikatoliki.
Lilianzishwa 1928 na padri Mhispania Josemaría Escrivá (1902-1975) mjini Madrid (Hispania). Sasa makao makuu yake yako Roma (Italia), na kiongozi wake ni askofu.
Ndani na nje ya Kanisa Katoliki kuna sifa tofauti kuhusu kazi ya kichungaji ya jimbo hilo.
Wapo wanaopinga mwelekeo wake wokisema Opus Dei inajaribu kutawala Kanisa na kufundisha aina ya Ukatoliki jinsi ilivyokuwa kabla ya Mtaguso wa pili wa Vatikano.
Kati ya wanaoiunga mkono, Papa Yohane Paulo II na mwandamizi wake Benedikto XVI walisifu kazi yake mara nyingi.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Opus Dei kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |