Wakamaldoli
Mandhari
(Elekezwa kutoka O.S.B.Cam.)
Wakamaldoli ni Wabenedikto wanaomfuata mkaapweke Romualdo Abati, mwanzilishi wa monasteri ya Camaldoli (Italia) katika karne ya 11.
Urekebisho huo wa umonaki wa Benedikto wa Nursia uliathiri vizuri sana Kanisa Katoliki hasa kupitia kardinali wake Petro Damiani aliyepigania urekebisho wa Kanisa lote kuanzia Upapa.
Kufuatana na himizo la Mtaguso wa pili wa Vatikano kwa wamonaki kuanzisha monasteri katika nchi za misheni, Wakamaldoli wa kike walifungua nyumba nchini Tanzania karibu na Mafinga (mkoa wa Iringa), ambayo kisha kustawi imeanza kuzaa matawi (mkoa wa Manyara).