Nenda kwa yaliyomo

Nyumba ya Mungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha la bwawa kutoka angani.

Nyumba ya Mungu ni bwawa linalozalisha umeme ambalo lipo katika wilaya ya Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, na kuenea katika wilaya ya Moshi pia.

Nyumba ya Mungu ipo kwenye bonde la mto Pangani; maji yake yanatoka katika Kikuletwa na Ruvu. Mito ya Kikuletwa na Ruvu hutiririsha takriban kilomita za mraba 7,500 (sq mi 2,900).

Lambo lilitengenezwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, kuzalisha umeme na viwanda vya samaki vilivyo kuwa karibu na pale. Madhumuni ya mwanzo ya kujenga bwawa hili yalikuwa kuhifadhi mtiririko wa mafuriko, ambayo yangeruhusu maendeleo ya ekari 30,000 za kilimo cha umwagiliaji na uzalishaji wa nishati ya umeme.

Kufikia mwaka 1970 bwawa hili lilikuwa na uzalishaji wa samaki wa Tilapia unaostawi. Hata hivyo, hii haikuchukua muda mrefu na ripoti zilizofuata kutoka mwaka 1972 mpaka 1973 zilionyesha kupungua kwa kiasi kikubwa cha bidhaa za samaki.

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyumba ya Mungu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.