Nyumba ya Chilenje 394
Mandhari
Nyumba ya Chilenje 394 ni makumbusho yanayopatikana katika eneo la Chilenje, Lusaka nchini Zambia.
Nyumba hiyo ilikuwa makazi ya Kenneth Kaunda aliyeishi hapo kuanzia Januari 1960 hadi Disemba 1962, na baadaye kuja kuwa rais wa kwanza wa nchi ya Zambia. Harakati za ukombozi wa uhuru nchini humo zilianzia katika nyumba hiyo hadi mafanikio ya taifa huru yalipopatikana tarehe 24 Oktoba 1964.[1]
Ni nyumba iliyogawanyika katika vyumba viwili vya kulala, sebule ndogo pamoja na jiko. Ni nyumba inayopatikana katika eneo ambalo miti yake inaonekana kustawi vizuri[2]
Tazama Pia
[hariri | hariri chanzo]- Makumbusho ya Reli (Zambia)
- Makumbusho ya Victoria (Maporomoko)
- Makumbusho ya Copperbelt
- Makumbusho ya Nayuma
- Makumbusho ya Taifa ya Lusaka
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Photo - Chilenje House 394, former house of Kenneth David Kaunda, now a small museum :: Pictures of Ridgeway, :: AllTravels :: Anywhere You Want To Go ::". alltravels.com. Iliwekwa mnamo 2014-04-19.
- ↑ "Uganda: In Chilenje House, the Kaunda Legacy Still Lives (Page 2 of 3)". allAfrica.com. 2012-12-05. Iliwekwa mnamo 2014-05-04.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyumba ya Chilenje 394 kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |