Nyanda za Juu za Adamawa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mazingira ya karibu na Ngaoundal katika Mkoa wa Adamwa wa Kamerun.

Nyanda za juu za Adamawa (kwa Kiingereza: Adamawa Plateau; Kifaransa: ['Massif de l'Adamaoua'] Error: {{Lang}}: text has malformed markup (help)) ni eneo la Afrika ya Kati linalopatikana kuanzia kusini-mashariki mwa Nigeria kupitia kaskazini mwa Kamerun (mikoa ya Adamawa na Kaskazini) hadi Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Jina la nyanda za juu hizo lilitolewa kwa kumbukumbu ya kiongozi Mwislamu wa Wafulani, Modibo Adama. Sehemu yake nchini Nigeria inajulikana pia kama Milima ya Gotel.

Nyanda za Juu za Adamawa ndizo chanzo cha mito mingi, pamoja na Mto Benue. Ni muhimu kwa madini yake ya boksiti. [1] Mwinuko wa wastani ni kama mita 1,000, [2] lakini mwinuko unaweza kufikia urefu wa mita 2,650. Uoto ni hasa savana, watu wanaoishi hapa ni wachache. Ufugaji wa ng'ombe ni kazi kuu katika eneo hilo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Encyclopædia Britannica - Adamawa Plateau. Jalada kutoka ya awali juu ya 15 October 2007. Iliwekwa mnamo September 15, 2007.
  2. MSN Encarta - Adamawa Plateau. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-10-31. Iliwekwa mnamo September 15, 2007.
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyanda za Juu za Adamawa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.