Ngudu
Ngudu ni kata ya Wilaya ya Kwimba katika Mkoa wa Mwanza, Tanzania. Msimbo wa posta ni 33801.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 32,446 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 27,630 waishio humo.[2]
Ni moja kati ya kata zinazokua kwa kasi kubwa ndani ya Wilaya ya Kwimba, ambayo ni wilaya kubwa zaidi mkoani Mwanza.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Kata ya Ngudu ndiyo inayoongoza katika maendeleo ukiilinganisha na kata nyingine wilayani Kwimba.
Inategemea kwa kiasi kikubwa ufugaji wa wanyama kama vile mbuzi, ng'ombe pamoja na kondoo, lakini pia kilimo ambacho kwa kiasi kikubwa hutumia jembe la mkono kuinua uchumi wa kata.
Mazao yanayolimwa katika kata ya Ngudu ni kama vile mpunga, mahindi pamoja na viazi vitamu.
Wakazi wengi hupendelea chakula aina ya michembe ambapo huweza kusaidia wakati wa uhaba wa chakula.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kata za Wilaya ya Kwimba - Mkoa wa Mwanza - Tanzania | ||
---|---|---|
Bugando | Bungulwa | Bupamwa | Fukalo | Hungumalwa | Igongwa | Ilula | Iseni | Kikubiji | Lyoma | Maligisu | Malya | Mantare | Mhande | Mwabomba | Mwagi | Mwakilyambiti | Mwamala | Mwandu | Mwang'halanga | Mwankulwe | Ng'hundi | Ngudu | Ngulla | Nkalalo | Nyambiti | Nyamilama | Shilembo | Sumve | Walla |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ngudu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |