Ngozi (mlima)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Ngozi (maana)

Kasoko na ziwa la Mlima Ngozi, Mbeya

Mlima Ngozi (pia: Ngosi) ni volkeno bwete katika safu ya milima ya Uporoto iliyopo kati ya miji ya Mbeya na Tukuyu nchini Tanzania.

Tangu kuporomoka kwa kichwa cha volkeno, Ngozi ina umbo la kasoko yenye ziwa ndani yake. Ziwa hili linalojulikana kwa jina la Ziwa Ngozi huhesabiwa kuwa ziwa la kasoko kubwa la pili barani Afrika.

Sehemu ya juu zaidi ya mlima ni mita 2,622 juu ya UB.

Mitelemko ya mlima upande wa kusini inafunikwa na misitu ya mvua yenye nyani aina ya mbega.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]