Ziwa Ngosi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ziwa Ngozi)
Ziwa Ngosi (Ngozi) ndani ya kasoko ya mlima wake.

Ziwa Ngosi (pia Ngozi) linapatikana kwenye milima ya Uporoto, Mkoa wa Mbeya nyanda za juu kusini mwa Tanzania. Ziwa hili limetokana na mlipuko wa volkeno, hivyo ni tofauti na maziwa mengine kama Ziwa Viktoria au Ziwa Nyasa. Upekee wa ziwa hili ni kwamba liko ndani ya kasoko ya mlima Ngozi na katikati ya misitu na lina urefu wa km 2.5, upana wake ni km 1.5, kina chake ni mita 74 na lina ukubwa wa hektari 9332.[1]

Maajabu mengine katika ziwa hili ni kwamba maji ya Ziwa Ngozi huwa lina muonekano wa rangi tofauti tofauti kila wakati, kuna wakati ukifika unakuta ziwa lina rangi ya samawati, kijani au nyeusi. Ni kwamba uwepo wa misitu husababisha rangi ya maji kubadilika na upande wa jua linapowaka.

Ndege hupendelea kuogelea pamoja na aina fulani ya bata huwa wanaogelea humo kwa wingi na kufanya ziwa kuwa na muonekano wa kupendeza zaidi.

Licha ya kuwa ziwa hilo linavutia kuangalia lakini halina samaki kama ilivyo katika maziwa mengine wala kuwa na historia ya uwepo wake na vilevile si rafiki kwa kuogelea.

Pia ziwa Ngosi lina maajabu ya kushangaza kwani mwonekano wake ni kama ramani ya bara la Afrika pamoja na visiwa vilivyopo Afrika mashariki ambavyo ni Pemba na Unguja.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]