Natanaeli wa Kana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Natanaeli kutoka Kana ya Galilaya ni mfuasi wa Yesu Kristo ambaye aliletwa kwake mapema na rafiki yake, Mtume Filipo, akaondolewa wasiwasi akamkiri kuwa Mwana wa Mungu, Mfalme wa Israeli (Injili ya Yohane 1:45-50.

Baada ya ufufuko wa Yesu, anatajwa tena (Yoh. 21:2) kuwa mmoja kati ya wanafunzi waliomfuata Mtume Petro kwenda ziwani kuvua samaki.

Wengi wanaona ni yuleyule ambaye katika Injili Ndugu anaitwa Bartolomayo, yaani mwana wa Tolomayo.