Wilaya ya Nachingwea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 07:54, 1 Oktoba 2020 na Kipala (majadiliano | michango) (kusahihisha msimbo wa posta, ni 653)
Mahali pa Nachingwea (kijani) katika mkoa wa Lindi.

Wilaya ya Nachingwea ni kati ya wilaya za Mkoa wa Lindi, yenye postikodi namba 653[1].

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 162,081 [1].

Wilaya hii imepakana na wilaya za Ruangwa upande wa kaskazini, Lindi Vijijini upande wa mashariki, halafu na mikoa ya Mtwara na Ruvuma upande wa kusini.

Nachingwea kuna hospitali, Chuo cha Ualimu, shule za sekondari 3 na za msingi 81 wilayani.

Eneo hili lilikuwa sehemu ya mradi wa karanga wakati wa ukoloni wa Uingereza.

Kuna madini ya nikeli katika Nachingwea na kampuni ya IMX Resources NL (zamani Goldstream Mining) kutoka Australia imeanzisha kampuni "Continental Nickel" ya kuchimba nikeli hiyo lakini hadi mwaka 2008 bado ilikuwa ikitafuta pesa kwenye soko la hisa la Kanada.

Asili ya Nachingwea

Neno Nachingwea asili yake ni mti mmoja uliokuwa ukiitwa Ngwea. Wakazi wa makao makuu ya wilaya ya Nachingwea wakati huo Ruponda walikuwa wakienda kuchota maji chini ya mti wa Ngwea, kwa hiyo walikuwa wakisema Nachi Ngwea wakimaanisha naenda kwenye Ngwea, maana yake nakwenda kuchota maji kwenye ngwea. Ndipo jina hilo Nachingwea likashika kasi na kuwa Nachingwea ya leo.

Makao makuu ya mwanzo ya Nachingwea yalikuwa Ruponda.

Viungo vya Nje

Marejeo

Kata za Wilaya ya Nachingwea - Mkoa wa Lindi - Tanzania

Boma | Chiola | Chiumbati Shuleni | Kiegei | Kilimanihewa | Kilimarondo | Kipara Mnero | Kipara Mtua | Lionja | Marambo | Matekwe | Mbondo | Mchonda | Mitumbati | Mkoka | Mkotokuyana | Mnero Miembeni | Mnero Ngongo | Mpiruka | Mtua | Nachingwea Mjini | Naipanga | Naipingo | Namapwia | Namatula | Nambambo | Namikango | Nang'ondo | Nangowe | Nditi | Ndomoni | Ngunichile | Raha leo | Ruponda | Stesheni | Ugawaji