Nenda kwa yaliyomo

Muwati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muwati
(Acacia spp.)
Muwati wa Madagaska
Muwati wa Madagaska
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Nusufamilia: Mimosoideae (Mimea inayofanana na kifauwongo)
Jenasi: Acacia (Miwati)
Mill., 1754
Ngazi za chini

Spishi >900, 16 katika Afrika:

"Majani" (vikonyo) ya muwati wa Madagaska

Miwati ni miti ya jenasi Acacia katika familia Fabaceae iliyo na majani yenye sehemu nyingi, lakini vikonyo vya majani vya spishi nyingi vimekuwa vipana na vimebadili majani menyewe. Zamani jenasi hii ilikuwa na spishi takriban 1300 lakini wanasayansi wameigawanya kwenye jenasi tano sasa: Acacia, Vachellia, Senegalia, Acaciella na Mariosousa[1]. Spishi za Acacia zinatofautiana na zile za jenasi Vachellia, Senegalia na Acaciella kwa ukosa wa miiba (ghairi ya muwati kangaruu). Hazina mastipula (majani mawili madogo chini ya jani kuu) kama spishi za Mariosousa.

Kwa asili takriban miti hii yote inatokea Australia lakini imewasilishwa katika mabara mengine. Hata hivyo spishi moja ni ya kienyeji ya Madagaska, spishi nyingine ya Reunion na spishi 12 za Asia.

Spishi ya Afrika (Madagaska na kisiwa cha Reunion)

[hariri | hariri chanzo]

Spishi zilizowasilishwa katika Afrika

[hariri | hariri chanzo]
  1. "The Acacia Debate". Science In Public. 2011. Iliwekwa mnamo 2011-08-03.