Nenda kwa yaliyomo

Mshonaji (ndege)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mshonaji
Kiota cha mshonaji katika majani yaliyoshonwa
Kiota cha mshonaji katika majani yaliyoshonwa
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Cisticolidae (Ndege walio na mnasaba na videnenda)
Sundevall
Ngazi za chini

Jenasi 4, spishi 23 za washonaji:

Washonaji ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Cisticolidae. Wamepewa jina hili kwa sababu ndege hawa huunganisha majani kwa kushona na kutengeneza tago lao ndani yao. Wana mkia mrefu uwekwao juu mara nyingi. Rangi yao ni kahawia, kijivu au kijani mgongoni na nyeupe, njano au kijivu isiyokolea chini; spishi kadhaa zina utosi mwekundu. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara na Asia ya tropiki katika misitu na mapori. Hula wadudu. Hulitengeneza tago kwa manyasi ndani ya majani yaliyoshonwa katika kichaka, mmea au kishungi cha manyasi. Jike huyataga mayai 2-3.

Spishi wa Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi wa Asia[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]