Mshonaji (ndege)
Mandhari
(Elekezwa kutoka Calamonastes)
Mshonaji | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kiota cha mshonaji katika majani yaliyoshonwa
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 4, spishi 23 za washonaji:
|
Washonaji ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Cisticolidae. Wamepewa jina hili kwa sababu ndege hawa huunganisha majani kwa kushona na kutengeneza tago lao ndani yao. Wana mkia mrefu uwekwao juu mara nyingi. Rangi yao ni kahawia, kijivu au kijani mgongoni na nyeupe, njano au kijivu isiyokolea chini; spishi kadhaa zina utosi mwekundu. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara na Asia ya tropiki katika misitu na mapori. Hula wadudu. Hulitengeneza tago kwa manyasi ndani ya majani yaliyoshonwa katika kichaka, mmea au kishungi cha manyasi. Jike huyataga mayai 2-3.
Spishi wa Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Artisornis metopias, Mshonaji Utosi-mwekundu (Red-capped Forest Warbler au African Tailorbird)
- Artisornis moreaui, Mshonaji Domo-refu (Long-billed Forest Warbler au Tailorbird)
- Calamonastes fasciolatus, Mshonaji Miraba (Barred Wren-Warbler)
- Calamonastes simplex, Mshonaji Kijivu (Grey Wren-Warbler)
- Calamonastes stierlingi, Mshonaji wa Stierling (Stierling's Wren-Warbler)
- Calamonastes undosus, Mshonaji-miyombo (Miombo Wren-Warbler)
- Camaroptera brachyura, Mshonaji Mgongo-kijani (Green-backed Camaroptera)
- Camaroptera brevicaudata, Mshonaji Mgongo-kijivu (Grey-backed Camaroptera)
- Camaroptera chloronota, Mshonaji Kijanikijivu Olive-green Camaroptera)
- Camaroptera harterti, Mshonaji wa Hartert (Hartert's Camaroptera)
- Camaroptera superciliaris, Mshonaji Nyusi-njano (Yellow-browed Camaroptera)
Spishi wa Asia
[hariri | hariri chanzo]- Orthotomus atrogularis (Dark-necked Tailorbird)
- Orthotomus castaneiceps (Philippine Tailorbird)
- Orthotomus chaktomuk (Cambodian Tailorbird)
- Orthotomus cinereiceps (White-eared Tailorbird)
- Orthotomus derbianus (Grey-backed Tailorbird)
- Orthotomus frontalis (Rufous-fronted Tailorbird)
- Orthotomus nigriceps (Black-headed au White-browed Tailorbird)
- Orthotomus ruficeps (Ashy Tailorbird)
- Orthotomus samarensis (Yellow-breasted Tailorbird)
- Orthotomus sepium (Olive-backed Tailorbird)
- Orthotomus sericeus (Rufous-tailed Tailorbird)
- Orthotomus sutorius (Common Tailorbird)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mshonaji miraba
-
Mshonaji kijivu
-
Mshonaji mgongo-kijani
-
Mshonaji mgongo-kijivu
-
Mshonaji kijanikijivu
-
Mshonaji nyusi-njano
-
Dume la dark-necked tailorbird
-
Jike la dark-necked tailorbird
-
Dume la ashy tailorbird
-
Jike la ashy tailorbird
-
Olive-backed tailorbird
-
Olive-backed tailorbird kando ya kiota chake ambamo yumo kinda la plaintive cuckoo
-
Rufous-tailed tailorbird
-
Common tailorbird
-
Common tailorbird