Msanidi programu
Makala hii, au sehemu za makala hii, inahitaji vyanzo au marejeo yoyote. Tafadhali saidia kuboresha makala hii kwa kuweka vyanzo vya kuaminika. Habari zisizowekewa vyanzo zinaweza kuwekewa alama na kuondolewa. |
Msanidi programu, au mhandisi programu, msanidi kompyuta au koda (kutoka Kiingereza programmer, computer programmer, software developer, software engineer au coder) ni mtu anayeunda programu za kompyuta[1].
Msanidi programu huunda programu ya kompyuta kwa kutoa maelekezo (kupitia lugha ya programu husika) kwa kompyuta, au kwa kusanidi msimbo chanzo uliopo. Wasanidi programu wengi wana uzoefu mkubwa kwenye mahesabu na uandishi wa misimbo chanzo kwa kutumia lugha za programu mbalimbali kama vile PHP, C, C++, Python, JavaScript, au SQL.
Wasanidi programu waliojikita kuunda programu za wavuti hupenda kujiita wasanidi wavuti (kutoka kwenye kiingereza web developer au web programmer).
Istilahi
[hariri | hariri chanzo]Hakuna neno rasmi lililoteuliwa, hivyo neno "msanidi programu" na "mhandisi programu" yanaweza kuwa na majukumu sawa kwenye baadhi ya makampuni, kwa kawaida mtu mwenye jina kazi la "msanidi programu" au "msanidi" kazi yake kubwa ni kubadili maelezo ya kina ya mfumo kuwa msimbo chanzo utakaoeleweka na kuchakatwa na kompyuta, kurekebisha makosa na kuhakiki msimbo chanzo. Anaweza kuwa na stashahada ya sayansi kompyuta, stashahada, aliyejifunza mwenyewe, au aliyehudhuria kambi zinazotoa masomo ya uandishi programu au mafunzo ya mtandaoni. Yule mwenye kazi jina la "mhandisi programu" anatarajiwa kuwa na uelewa mpana kuhusu sheria na kanuni za uhandisi, hisabati na njia za kisayansi.
Historia
[hariri | hariri chanzo]
Mwanahisabati wa kiingereza Ada Lovelace, ndiye anayetambulika na wengi kama msanidi wa kwanza wa programu kwasababu aliandika algoriti ya kwanza ya kukokotoa nambari za Bernoulli, algoriti iliyopaswa kuchakatwa na injini ya uchanganuzi ya Charles Babbage [2] ambayo kwa wakati huo ilikua bado haijaundwa.
Wanachama wa timu ya upangaji programu (Kingereza: programming) ya ENIAC ya mwaka 1945, Kay McNulty, Betty Jennings, Betty Snyder, Marlyn Wescoff, Fran Bilas na Ruth Lichterman, ndiyo wanajulikana kama wasanidi programu wa kwanza wa kulipwa.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Programmer Definition & Meaning | Britannica Dictionary". www.britannica.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-07.
- ↑ "Lovelace & Babbage and the creation of the 1843 'notes' | IEEE Journals & Magazine | IEEE Xplore". ieeexplore.ieee.org. Iliwekwa mnamo 2024-01-08.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Msanidi programu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |