Nenda kwa yaliyomo

ENIAC

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

ENIAC (kifupisho cha Electronic Numerical Integrator and Computer) ni tarakilishi au kompyuta za kwanza katika historia ya kompyuta.

Ilikuwa na uwezo wa kufanya mahesabu na ilikuwa na kasi ndogo sana. Kwa mara ya kwanza ilitengenezwa katika chuo cha Pennsylvania tarehe 15 Februari 1946.

Matengenezo ya ENIAC yalidhaminiwa na jeshi la Marekani Likiongozwa na meja jenerali Gladeon M. Barnes. Matengenezo haya yaligharimu takribani dola za Kimarekani 487,000, ambazo ni sawa na dola 6,740,000 za mwaka 2016.

Mkataba wa kazi hiyo ulitiwa sahihi tarehe 5 Juni 1943. Kazi hii ilianzishwa kwa siri katika chuo cha Pennsylvania, idara ya uhandisi wa umeme.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.