Nenda kwa yaliyomo

Msambiazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Msambiazi ilikuwa kata ya Wilaya ya Korogwe katika Mkoa wa Tanga, Tanzania.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,541 waishio humo[1].

Kijiji cha Msambiazi ni muunganiko wa vijiji vikubwa vitatu: Msumbiji, Migombani na Msambiazi yenyewe. Pia Msambiazi ni njia panda ya kwenda Lewa na Lutindi ambako kuna Hospitali ya vichaa.

Wenyeji wa Msambiazi ni Wazigua ambao wengi wamefanya kuhamia hapo toka maeneo ya vijiji vya mbali, ng'ambo ya mto Ruvu, kama Kwasigi, Antakae, Relini n.k. walihamishiwa hapa na serikali kipindi cha kujenga vijiji vya Ujamaa. Pia kuna Wasambaa na Wabondei ambao idadi yao imeongezeka kutokana na kuoana na shughuli za biashara.

  1. "2002 Population and Housing Census General Report" (kwa Kiingereza). Government of Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-03-18. Iliwekwa mnamo 2008-08-21.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Msambiazi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.