Nenda kwa yaliyomo

Moshi William

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanamuziki Moshi William wakati wa uhai wake. Picha kwa hisani ya Muhiddin Issa Michuzi.

TX Moshi William (jina halisi: Shaban Ally Mhoja Kishiwa) alikuwa mmoja wa wanamuziki mahiri wa muziki wa dansi kutoka Tanzania aliyeweza kurekodi albamu 13.

Alizaliwa Tanga mwaka 1958 na alifariki dunia tarehe 29 Machi mwaka 2006, akiacha mke mmoja na watoto wanne.

Kwa miaka mitatu mfululizo (2003, 2004, 2005) Moshi William alitunukiwa tuzo ya kitaifa ya utunzi bora.

Alijiunga na bendi kongwe kutoka Tanzania Juwata Jazz Band mwaka 1982 akitokea bendi ya Polisi Jazz.

Mwanamuziki huyo alijipatia umaarufu mkubwa kwa kutunga nyimbo zilizokuWa na mafunzo katika jamii, mfano wa nyimbo kama Ashibae, Mwaka wa Watoto, Msafiri Kakiri, Asha Mwanaseifu, Kaza Moyo, Ajuza, Ndoa Ndoano, Mwanamkiwa, Ajali, Nyongo Mkaa na Ini, Isihaka Kibene, Harusi ya Kibene, Piga Ua Talaka Utatoa na nyimbo nyingine nyingi.

Ukipita mitaa ya Keko Machungwa jijini Dar es Salaam sehemu alikokuwa anaishi mwanamuziki huyu lazima utasikia moja ya nyimbo zake zikipigwa katika vilabu mbalimbali au kwenye majumba ya wenyeji. Pia katika miji mbalimbali ya Afrika Mashariki na kati mwanamuziki huyu alifananishwa sana na mwanamuziki Madilu System wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na staili yake ya uimbaji katika Bendi ya Msondo Ngoma na mtoto wake Hassan Moshi William.

Kifo cha mwanamuziki Moshi William kiliacha pengo kubwa katika bendi ya Msondo Ngoma.

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Moshi William kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.